Tanzania ya kwanza Afrika kutumia Mashine ya kufuatilia wagonjwa nyumbani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila mashine ya Dozee iliyotengenezwa na Sakaar Health Tech LTD ambayo inatumika kuwafuatilia wagonjwa wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika.
***********************************************************************************************************************************************************************************
Kwa mara ya kwanza barani Afrika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Sakaar Health Tech LTD wamezindua rasmi mashine maalum itakayotumika kufuatilia wagonjwa wa moyo wakiwa nyumbani ili kujua hali zao na kutoa msaada wa haraka endapo utahitajika.
Kufuatia uzindunzi wa mashine hiyo iitwayo Dozee Tanzania sasa imekuwa nchi ya tatu Duniani kutoa huduma hivyo huku ikiwa nchi ya kwanza barani Afrika.
Mhe. Chalamila alisema Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza kwa kiasi kikubwa katika afya ya watanzania ili kuhakikisha kuwa na watu ambao wana afya bora na kuweza kuwa na mchango wa kuleta maendeleo.
“Serikali imefanya mambo mengi ukiende kwenye uzazi amepunguza vifo lakini amejengea uwezo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (KCI) na magonjwa ya moyo yapo kazi iliyopo ni kuhakikisha tunakabiliana nayo kwa kuwekeza kwenye teknoloji.
Pia ameipongeza Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kumuunga mkono Mhe. Rais Samia ikiwa na ubunifu huo wa kuendelea kutoa huduma kwa wananchi .
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge alisema ili kwenda na teknoloji na kuwahudumia wananchi wamekuja na njia mbadala ya kisasa ya kuhudumia wagonjwa nyumbani mara watakapofanyiwa upasuaji au kufanyiwa tiba hapo JKCI kama upasuaji mdogo wa moyo ka kutumia mtambo wa Cathlab.
“Sasa kwa hawa wagonjwa mara nyingine wanabadilika mapigo ya moyo yanakwenda kasi sana kwahiyo tunachofanya hii Dozee inawekwa chini ya kitanda na unaweza kugundua mapigo yao ya moyo na presha na jinsi wanavyopumua na kama kukitokea tatizo unaweza kugundua.
Aliongeza, “Hivi juzi kuna mgonjwa alitibiwa kwetu tukamwekea Dozee usiku mapigo ya moyo yakapanda hadi 140 na wakati mwingine 160 tukapata alarm tukampigia simu na tukarudisha na sasa anaendelea na matibabu”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge ambaye pia ni daktari bingwa wa moyo alisema teknolojia hiyo itasaidia kuwahudumia wagonjwa vilevile itapunguzia gharama kwa ambao walikuwa walazwe hospitalini kwa wiki mbili sasa wanakaa siku tano na baade kufuatiliwa wakiwa nyumbani.
Comments
Post a Comment