Wanafunzi UDSM watoa zawadi kwa watoto wenye matatizo ya moyo na kuchangia damu chupa 14
Mwanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka wa Tatu anayesomea Biashara upande wa Masoko Giveness Kitale akimkabidhi zawadi mama wa mtoto aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya matibabu ya moyo. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu.
Mwanachuo wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) anayesomea Biashara upande wa Masoko George Temba akimkabdhi zawadi za watoto waliolazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Afisa Muuguzi Msaidizi Grace Sanga. Wanachuo hao wa UDSM walitembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia damu.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joseph Mwalongo akiwaeleza wanafunzi wanaosomea Biashara upande wa Masoko kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) kuhusu magonjwa ya moyo kwa watoto wakati wanafunzi hao walipotembelea JKCI hivi karibuni kwaajili ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika Taasisi hiyo pamoja na kuchangia damu.
Wanachuo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wanaosomea Biashara upande wa Masoko wakichangia damu kwaajili ya watoto wanaofanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wanachuo hao walichangia chupa 14 za damu pamoja na kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika taasisi hiyo.
Comments
Post a Comment