Wahandisi wafanyiwa vipimo vya viashiria magonjwa ya moyo
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Faizat
Ndosa akimpima sukari kwenye damu mhandisi aliyetembelea banda la JKCI wakati
wa mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa) unaofanyika katika
ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere International Convention Center (JNICC)
uliopo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa huduma za afya za mtandao kutoka kampuni ya
Cloudscript inayofanya kazi na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Beatrice
Mmari akiwafundisha wahandisi namna ya kutumia huduma ya afya mtandao kupitia
mfumo wa Cloudscript walipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano wa 30 wa
wahandisi washauri Afrika (FIDIC Africa) unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa
wa Mwalimu Nyerere International Convention Center (JNICC) uliopo jijini Dar es
Salaam.
Na: JKCI
*********************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatoa huduma za
uchunguzi wa magonjwa ya moyo na ushauri wa lishe bora kwa wahandisi kutoka
nchi za Afrika walioudhuria mkutano wa 30 wa wahandisi washauri Afrika (FIDIC
Africa).
Huduma hiyo inatolewa kwa siku mbili katika viwanja vya
ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Julius Nyerere International Convention Center (JNICC)
vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia huduma hiyo daktari kutoka Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli George alisema JKCI imeona umuhimu wa kuwasogezea
wahandisi huduma za uchunguzi wa magonjwa ya moyo karibu kuwapa nafasi ya
kuchunguza afya zao.
“Waandisi muda mwingi wanakuwa katika maeneo yao ya kazi
(site) na kukosa nafasi ya kufika Hosptitali kwaajili ya kuchunguza afya hivyo
kupitia mkutano huu tunawapa nafasi ya kupima afya lakini pia tunawapa elimu ya
namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo”, alisema Samweli
Katika kutoa elimu ya mfumo bora wa maisha Dkt. Samweli
aliwataka wahandishi kuwa na tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara na
kuijua miili yao kwani magonjwa ya moyo wakati mwingine humtokea mtu bila ya
kuonyesha dalili.
Kwa upande wake Mhandisi kutoka Tanroad Magdalena Evance
aliwashukuru wataalamu wa afya kutoka JKCI kwa kumfanyia uchunguzi wa afya
kwani hajawahi kuchunguza afya yake kama hana changamoto yoyote ya ugonjwa.
“Leo nimejifunza kitu kikubwa sana katika maisha yangu,
natakiwa kuchunguza afya yangu kila ninapopata nafasi na nisisubiri hadi niumwe
kwasababu tumeambiwa magonjwa yasiyoambukiza wakati mwingine hayana dalili”,
alisema Magdalena
Magdalena alisema baada ya kupima amepata ushauri wa namna ya
kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza elimu ambayo ataizingatia kwani kinga ni
bora kuliko tiba.
Comments
Post a Comment