Banda la JKCI lawavutia wananchi kupima moyo
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Zuhura Yunus akiwa katika picha ya Pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la JKCI kwaajili ya kuangalia huduma wanazozitoa katika maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika katika viwanja vya Mandewa mkoani Singida. Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Joseph akimpima shinikizo la damu (BP) mkazi wa Singida aliyefika katika viwanja vya maonesho Mandewa kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa bila malipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa Kazi. Mkurugenzi wa Usalama na Afya kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) Dkt. Jerome Materu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa maonesho ya Kimataifa ya Wiki ya Usalama na Afya Mahali Pa kazi yanayofanyika k...