Furaha ya watani wa jadi, uhakika wa Afya: Mashabiki wa Simba na Yanga kupimwa moyo bure
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na mashabiki wa timu za mpira wa miguu za Simba
na Yanga kuhusu upimaji utakaofanyika kwa mashabiki hao wakati wa mechi
itakayofanyika siku ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja wa Mpira
wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Young Africans (Yanga)
Ally Kamwe akiwahamasisha mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kufanya uchunguzi
wa afya utakaofanywa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa mechi
ya Simba na Yanga siku ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja wa
Mpira wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba Sports Club Ahmed Ally akitoa neno la shukrani kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa mashabiki wa timu za Simba na Yanga wakati wa mechi itakayofanyika siku ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mashabiki wa timu za mpira wa miguu za Simba na
Yanga wakifuatilia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu huduma
za upimaji na matibabu ya moyo zitakazotolewa wakati wa mechi ya timu hizo siku
ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya mashabiki wa timu za mpira wa miguu za Simba na
Yanga wakifuatilia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu huduma
za upimaji na matibabu ya moyo zitakazotolewa wakati wa mechi ya timu hizo siku
ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo
Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya mpira
wa miguu ya Simba Sports Club mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishi
wa habari kuhusu upimaji wa magonjwa ya moyo utakaofanyika wakati wa mechi ya Simba na Yanga siku ya
jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja
wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na mashabiki wa timu ya mpira
wa miguu ya Young African (Yanga) mara baada ya kumalizika kwa mkutano na
waandishi wa habari kuhusu upimaji wa magonjwa ya moyo utakaofanyika wakati wa
mechi ya Simba na Yanga siku ya jumapili tarehe 21 Disemba 2025 katika Uwanja
wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Picha na: JKCI
Upimaji huo utakaotolewa bila gharama pia utafanyika kwa kila
mwananchi atakayefika katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa KMC uliopo Kijitonyama
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema
JKCI imeona ichukue jukumu la kufika katika Uwanja wa KMC wakati wa mechi hiyo
kutoa huduma kwa wananchi kwani wengi wao hawana tabia ya kuchunguza afya mara
kwa mara.
“Magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo yanaongezeka kwa
kasi, tumechukua jukumu la kuwafuata mashabiki na wachezaji wa timu hizi kubwa
ili tuweze kuwapima na kuwapa elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza” alisema
Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa
na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza wataalamu wa afya na vifaa tiba
hivyo siku ya mechi hiyo JKCI itakuwa na vifaa vinavyotumia akili unde
kuchunguza moyo unavyofanya kazi.
“Huduma hii imetolewa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa
mashabiki wa timu hizi ili wanapokuwa na furaha kushabikia timu zao basi wawe
na uhakika wa afya zao”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake msemaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba
Sports Club Ahmed Ally alisema mwanzoni wakati mechi hiyo ikiandaliwa ilikuwa
na kusudi la watu kwenda kupata burudani lakini jambo hilo limeongezeka thamani
na kutoa fursa kwa mashabiki wa timu hizo kupata huduma za afya.
Ahmed alisema kwa wale ambao wamepitia changamoto za kuugua
ama kuuguza wanafahamu thamani ya kupata vipimo na matibabu kutoka kwa
wataalamu mabigwa wabobezi, hivyo mashabiki hao watumie vizuri fursa hiyo
adhimu ambayo imewafikia kirahisi.
“Kupitia mechi yetu ya Simba na Yanga tunaenda kapata vipimo
na matibabu ya moyo kwa haraka, bila gharama zozote, nauli yako utakayotoka
nayo nyumbani ndio itakuwezesha kufanya uchunguzi wa afya chini ya wataalamu
bingwa kutoka JKCI”, alisema Ahmed
Naye msemaji wa timu ya mpira wa miguu ya Young Africans
(YANGA) Ally Kamwe alisema mashabiki wa Yanga wameshukuru kwa fursa ambayo JKCI
imeitoa kwao kwani mchezo kati ya timu hizo unahusisha hisia kubwa ambayo
inaweza wasababishia mashabiki kupata magonjwa ya shinikizo la damu.
“Kwa nafasi yenu mmeamua kuitumia mechi hii ya mashabiki wa
Yanga na Simba kutoa huduma za matibabu ya moyo bila gharama, tunawashukuru
sana, mwanzoni tuliona ni mechi ya kawaida kumbe ni mechi ambayo inaenda
kusaidia jamii yenye uhitaji wa uchunguzi na matibabu ya moyo”, alisema Ally
“Mashabiki wa Yanga
tunapata raha lakini kucheki afya pia ni muhimu, kwani tunaweza kuwa tunapata
raha Yanga lakini furaha hiyo inaweza kuharibiwa katika maeneo yetu mengine na
kutusababishia shida za moyo, fursa hii tuitumie vizuri”, alisema Ally
Upimaji huo utakaonza kutolewa kukanzia saa mbili asubuhi
siku ya Jumapili utahusisha wataalamu mabingwa wa magonjwa yasiyoambukiza na
wataalamu wa lishe huku ukienda na Kauli mbiu isemayo “pima moyo wako leo uishi
kesho, jitokeze kupima”,.







Comments
Post a Comment