Mashabiki 175 wa Simba na Yanga wapimwa afya ya moyo
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na Mkurugenzi wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa JKCI Dkt. Tatizo Waane wakizungumza na mmoja wa mashabiki wa timu ya Simba wakati wa upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanywa na Taasisi hiyo kabla ya mechi ya mpira wa miguu baina ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima moyo wakati wa kambi maalumu iliyofanywa na Taasisi hiyo jana kabla ya mechi ya mpira wa miguu kati ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga iliyofanyika katika uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa vipimo vya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Emily Joseph akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mwananchi aliyefika katika banda la JKCI kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa mashabiki wa timu za Simba na Yanga jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dotto Sebastian akimsikiliza mwananchi alifika katika banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya uchuguzi na matibabu ya moyo kwa mashabiki wa timu za mpira za Simba na Yanga kabla ya kuanza kwa mechi yao jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Justine akimpima mapigo ya moyo mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na JKCI kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu baina ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimfafanulia mwananchi kuhusu magonjwa ya moyo mara baada ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu iliyofanywa na Taasisi hiyo kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu baina ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Afisa Muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Ester Paschal akimpima uwiano baina ya urefu na uzito shabiki wa Simba wakati wa kambi maalumu ya uchuguzi na matibabu ya moyo iliyokuwa ikifanywa na JKCI kwa mashabiki wa timu za mpira za Simba na Yanga kabla ya kuanza kwa mechi yao jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Morris Budotela akimshauri mwananchi aliyefika kupata huduma katika kambi maalumu ya uchunguzi na matibabu ya moyo kabla ya kuanza kwa mechi ya mpira wa miguu baina ya mashabiki wa timu za Simba na Yanga jana katika Uwanja wa mpira wa KMC uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
**********************************************************************************************************************************************************************************************************************
Kambi hiyo ilifanyika jana sambamba na mechi ya mashabiki wa timu hizo
katika Uwanja wa Mpira wa Miguu wa KMC
uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam,
ambapo mashabiki walipatiwa vipimo mbalimbali vya afya ya moyo ikiwemo kupima
uwiano wa urefu na uzito.
Vipimo vingine vilivyotolewa ni pamoja na
kipimo cha kiwango cha sukari kwenye damu, shinikizo la damu na mapigo ya moyo,
kipimo cha mfumo wa umeme wa moyo (ECG) pamoja na kipimo cha kuangalia utendaji
wa moyo (ECHO).
Akizungumza wakati wa zoezi hilo Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge
alisema kambi hiyo imelenga kuwasaidia
mashabiki kufuatilia afya zao za moyo huku wakiendelea kufurahia michezo
wanayoipenda.
“Nimefurahi kuona
washabiki wengi wa Simba na Yanga wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao. Ninawaomba
wanapopata fursa kama hizi, wazitumie vizuri ili kujitambua kiafya na kupata
elimu ya namna ya kujikinga na magonjwa ya moyo,” alisema Dkt. Kisenge.
Kwa upande wake daktari kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari alisema watu 12 wamepewa rufaa ya kufika katika
taasisi hiyo kwa ajili ya uchunguzi wa kina zaidi baada ya kubainika kuwa na
changamoto za kiafya.
“Waliopata rufaa
wapo waliobainika kuwa na shinikizo la juu la damu, huku mmoja akigundulika
kuwa na ugonjwa wa kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo. Wakifika JKCI tutafanya
vipimo zaidi na kuwashauri hatua sahihi za matibabu,” alisema Dkt. Janeth.
Aliongeza kuwa washiriki wote waliopimwa
wamepewa elimu ya kujikinga na magonjwa ya moyo kwa kuepuka vichochezi
hatarishi kama uvutaji wa sigara,
matumizi ya pombe kupita kiasi, pamoja na kuzingatia lishe bora na
mazoezi ya mara kwa mara.
“Wapo tuliowakuta
na shinikizo la juu la damu bila wao kujijua, jambo linaloonesha umuhimu wa
kupima afya mara kwa mara,”
alisisitiza.
Nao mashabiki wa Simba na Yanga waliipongeza Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwafuata wananchi moja kwa moja katika
maeneo ya mikusanyiko na kuwapatia huduma za uchunguzi wa afya bila usumbufu wa
kufika hospitalini.
Jonas Ibrahimu, shabiki wa Simba alisema elimu aliyopata ya jinsi ya kujikinga
na magonjwa ya moyo itamsaidia kubadili mtindo wa maisha kwa kuacha tabia
hatarishi, kufanya mazoezi na kuzingatia lishe bora.
Kwa upande wake Juma Said shabiki wa Yanga, aliomba JKCI kuendeleza kambi kama hizo katika matukio mbalimbali ya michezo na maeneo mengine ya mikusanyiko huku akisema akisema hatua hiyo ina mchango mkubwa katika kuimarisha afya ya jamii na kuokoa maisha ya Watanzania.







Comments
Post a Comment