JKCI kufungua tawi DRC Congo

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Said Juma Mshana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo nchini Tanzania Mhe. Prof. Jean Pierre Massala walipotembela Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.

Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Said Juma Mshana akielezea dhumuni la ziara ya Gavana wa jimbo la Maniema nchini Congo Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.


Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza wakati wa ziara ya Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alipotembelea taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.

Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise akiwa katika picha ya pamoja na viongozi kutoka nchini Congo na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma zinazotolewa pamoja na kuangalia namna ya kushirikiana na Taasisi hiyo kukuza huduma za moyo nchini Congo.

Na JKCI

**********************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) imepanga kuvuka mipaka ya nchi na kufungua tawi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika kutoa huduma bingwa bobezi za matibabu ya moyo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt Peter Kisenge wakati wa ziara ya Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alipotembelea JKCI leo jijini Dar es Salaam.

Dkt. Kisenge alisema JKCI inataka kusogeza huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa Congo kuwapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kwenda katika mataifa ya mbali kupata huduma hizo.

“Tunawaahidi watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa tutatoa ushirikiano na kuwasaidi wasitumie gharama nyingi ambazo wanazitumia kupeleka wagonjwa nje ya Afrika kwa kuwasogozea huduma hizo karibu” alisema Dkt. Kisenge

Kwa upande wake Gavana wa jimbo la Maniema la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Mussa Kabwankubi Moise alisema baada ya kutembelea Taasisi hiyo ameridhishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ya Tanzania na kuifanya JKCI kuwa kinara katika utoaji wa huduma bingwa bobezi za upasuaji wa moyo Afrika Mashariki na kati.

“Nimevutiwa sana na ubora wa huduma zinazotolewa na JKCI ni jambo la kujivunia kuona Taasisi ya Serikali ikitoa huduma za kiwango cha juu namna hii”, alisema Mhe. Moise

Mhe. Moise aliongeza kuwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itashirikiana na JKCI kwa kuwaleta wagonjwa waliokuwa wakipelekwa nje ya nchi kutibiwa ili waweze kupunguza gharama zinazotumiwa na Serikali hiyo kuwasafirisha watu wake kwa ajili ya matibabu ya moyo katika nchi za mbali. 

Naye Balozi wa Tanzania katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Juma Saidi Mshana   aliipongeza menejimenti ya Taasisi hiyo kwa kushirikiana vema na nchi ya Congo katika kuimarisha uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi  hizo mbili.


Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi