JKCI na Poland: Fursa mpya za Utafiti, Ujuzi na "Grants"


Balozi wa Poland nchini Tanzania Mhe. Sergiusz Wolski akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland walipotembelea ubalozi huo leo kwaajili ya kuona namba watakavyofanya  ushirikiano na JKCI katika masuala ya utafiti, ujuzi na “grants”.

Balozi wa Poland nchini Tanzania Mhe. Sergiusz Wolski akizungumza na ujumbe kutoka chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland walipotembelea ubalozi huo leo kwaajili ya kuona namna ya kufanya ushirikiano na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) katika masuala ya utafiti, ujuzi na “grants”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati wa kikao na Balozi wa Poland nchini Tanzania Mhe. Sergiusz Wolski kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam cha kujadili namna Taasisi hiyo itakavyoshirikiana na Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland katika masuala ya utafiti, ujuzi na “grants”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi mtaalamu kutoka Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland Mateusz Wylaz mara baada ya kutembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kuona namna watakavyoshirikiana  katika masuala ya utafiti, ujuzi na “grants”

Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group, Dkt. Tulizo Shemu akimpa zawadi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jagiellonian kilichopo nchini Poland Prof. Bartlomiej Guzik mara baada ya kutembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona namna watakavyofanya ushirikiano  katika masuala ya utafiti, ujuzi na “grants”.

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na Burkina Faso zasaini makubaliano ya ushirikiano katika kutoa tiba ya magonjwa ya moyo

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Msumbiji kushirikiana na JKCI katika tiba ya moyo