Watu zaidi ya 300 wafanyiwa uchunguzi wa afya na JKCI Tamasha la IST Festival
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Tamasha la IST Festival lililofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Daktari
wa kinywa na meno wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar
Group Aitham Mohamed akimfanyia uchunguzi wa kinywa mwananchi aliyetembelea
banda la Hospitali hiyo kwaajili ya kupata huduma wakati wa Tamasha la IST Festival
lililofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fakihi Mguwalo akimpima shinikizo
la damu (BP) Mkurugenzi wa Halmashauri jiji la Dar es Salaam Elihuruma Mabelya
aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Tamasha la IST Festival
lililofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini Dar es
Salaam.
Afisa huduma kwa wateja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stephano Zavara akitoa elimu kuhusu afya ya moyo kwa wananchi waliotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Tamasha la IST Festival linalofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kliniki ya Kawe Flora Zakaria akimpima
shinikizo la damu mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa Tamasha
la IST Festival lililofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini
Dar es Salaam.
Daktari
bingwa wa macho wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group
Festus Mhagama akimpima kipimo cha kuangalia macho mwananchi aliyetembelea
banda la Hospitali hiyo wakati wa Tamasha la IST Festival lililofanyika jana
katika viwanja vya Coco Beach vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Watu zaidi ya 300
wafanyiwa uchunguzi wa afya na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa
tamasha la IST Festival lililofanyika jana katika viwanja vya Coco Beach
vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Watu hao wamefanyiwa
uchunguzi wa afya kwa kufanyiwa vipomo vya kuangalia viashiria vya magonjwa ya
moyo, kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (ECHO), Kipimo cha
kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (ECG), kipimo cha kuangalia magonjwa ya macho
na kipimo cha kuangalia afya ya kinywa na meno.
Akizungumza wakati wa
Tamasha hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge alisema katika Tamasha hilo JKCI ilikuwa na kauli mbiu isemayo
“Jua namba zako ikiwemo shinikizo la damu, sukari kwenye damu, na mapigo ya
moyo” kuihamasisha jamii kuweza kujifahamu na kutambua viashiria vya magonjwa
yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo.
“Kupitia kauli mbiu yetu
tunataka kila kijana aliyeshiriki katika Tamasha hili anapoondoka aende na
ujumbe huu kwa vijana wenzake ili kwa pamoja tuweze kuzuia magonjwa ya moyo
ambayo yamekuwa tishio katika jamii zetu”, alisema Dkt. Kisenge
Dkt. Kisenge alisema
asilimia 10 ya wagonjwa wote waliofanyiwa uchunguzi wa afya katika banda la
JKCI wamekutwa na magonjwa mbalimbali yakiongozwa na magonjwa ya kinywa na meno
hivyo kuwakata watu hao kufika katika Taasisi hiyo kwaajili ya matibabu zaidi.
“Watu wote waliokutwa
na matatizo mbalimbali kupitia tamasha hili wafike katika Taasisi yetu tutawapa
huduma bila gharama ili tuweze kutatua matatizo yao ambayo wengi wao hawakuwa
wanafahamu kama wanayo”, alisema Dkt. Kisenge
Kwa upande wake Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila alisema kutokana na JKCI kutumia
wataalamu wake mara kwa mara kufikisha huduma za uchunguzi wa afya kwa jamii
ofisi yake itatoa kiasi cha Tshs. Milioni 200 kama sehemu ya kuwezesha
uchunguzi wa afya kwa kuwafuata wananchi mahali walipo.
Mhe. Chalamila alisema
JKCI imefanya kazi kubwa kupitia Tamasha hilo kwani kwa pamoja waliona
wakiishia kufanya tamasha tu bila upimaji wangekuwa hawajawafikia wananchi na
kuwasaidia ndio maana wakatoa huduma hizo za afya bila gharama.
Aidha Mhe. Chalamila
aliitaka jamii kujitokeza kwa wingi kukata bima ya afya kwa wote itakayowasaidia
kujilinda wakati wanahitaji kupata huduma za afya kwani bima hiyo itawawezesha
kupata huduma katika hospitali kubwa ikiwemo JKCI.
“Nimefika JKCI nimeona
mazingira yalivyo mazuri, Serikali imewekeza sana katika Taasisi hii kwani ni
mabingwa kweli kweli, mkiwa na bima za afya mtaweza kupatiwa huduma katika
Taasisi hii”, alisema Mhe. Chalamila
Nao wananchi waliopata
huduma katika banda la JKCI waliishukuru Taasisi hiyo kwa kuwafikia wananchi na
kupata huduma na elimu kuhusu namna ya kujikinga na magonjwa hayo kwani watu
wengi hawana ufahamu wa kutosha kuhusiana na magonjwa ya moyo.
Denis Robert alisema
amekuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo ambalo alishatibiwa lakini kupitia
tamasha hilo ameweza kukutana na wataalamu wa JKCI ambao baada ya kumfanyia
uchunguzi wamemwambia anaendelea vizuri.
Fatuma Athumani alisema
ametembelea banda la JKCI na kufanya uchunguzi wa macho na meno ambapo
ameambiwa ana shida kidogo kwenye meno hivyo kupewa rufaa kufika katika Taasisi
hiyo tawi la Dar Group kwaajili ya uchunguzi zaidi.
Naye Jumanne Kulwa
alisema baada ya kuona tangazo kupitia TV aliona na siku nzuri ya kuonesha
upendo ambapo JKCI imeonesha upendo kwa kuwapatia huduma za uchunguzi na
matibabu ya afya wananchi ndio maana na yeye akafika ili aweze kuchunguza afya
yake.
Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) imekuwa na taratibu ya kufanya kambi mbalimbali za uchunguzi na
matibabu ya magonjwa ya moyo katika mikoa zaidi ya 23 lengo likiwa kusogeza
huduma karibu na wananchi lakini pia kutoa elimu kwa jamii ya namna ya kujikinga
na magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)



Comments
Post a Comment