Wataalamu kutoka nchini Namibia watembelea JKCI kuona huduma zinazotolewa
Mkurugenzi wa Idara ya
Upasuaji wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya
akimpatia zawadi Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Uwekezaji na Maendeleo ya
nchini Namibia (NIPDB) Jessica Hauuanga wakati wataalamu kutoka nchini Namibia
walipofanya ziara katika Taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona namna
watashirikiana katika kutoa huduma za matibabu ya moyo kwa wananchi wa Namibia.
Fundi Sanifu wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Kulindwa Kasubi akielezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji mdogo wa moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab kwa wajumbe kutoka nchini Namibia walipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona huduma zinazotolewa ili wagonjwa kutoka nchini Namibia waanze kupata huduma katika Taasisi hiyo.
Daktari bingwa wa
upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Alex Joseph akizungumza na ujumbe kutoka nchini Namibia walipotembelea Taasisi
hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona huduma zinazotolewa ili wagonjwa kutoka
nchini Namibia waanze kupata huduma katika Taasisi hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha
Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Thadei Kavishe akiwaeleza
wajumbe kutoka nchini Namibia jinsi maabara ya kisasa inayotumia akili unde
(AI) inavyofanyakazi wakati ujumbe huo ulipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya
kujifunza na kuona huduma zinazotolewa ili wagonjwa kutoka nchini Namibia
waanze kupata huduma katika Taasisi hiyo.
Mkurugenzi Idara ya
Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akieleza huduma
zinavyotolewa katika Idara ya Uuguzi kwa ujumbe kutoka nchini Namibia walipotembelea
Taasisi hiyo kwaajili ya kujifunza na kuona huduma zinazotolewa ili wagonjwa
kutoka nchini Namibia waanze kupata huduma katika Taasisi hiyo.
Na JKCI
**************************************************************************************************
Ujumbe wa viongozi, wataalamu
wa afya na wafanyabiashara kutoka nchini Namibia watembelea Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) kuangalia huduma zinazotolewa pamoja na kujifunza ili
iweze kuanzisha ushirikiano wa kuwaleta wagonjwa wa nchini humo kupata huduma
katika Taasisi hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter
Kisenge, Mkurugenzi wa Idara ya Upasuaji wa JKCI Dkt. Angela Muhozya alisema wataalamu
hao wameweza kujifunza na kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali katika
Taasisi hiyo.
“Nchini Namibia hakuna Taasisi
kama yetu inayotoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo hivyo wakaona ni
muhimu wakaja kujifunza kwetu na kuangalia namna ya kushirikiana katika kutoa
huduma bingwa bobezi za moyo kwa wananchi wa Namibia”, alisema Dkt. Angela.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji
Mkuu wa Bodi ya Uwekezaji na Maendeleo kutoka nchini Namibia (NIPDB) Jessica
Hauuanga alisema maendeleo yaliyopo katika Sekta ya Afya nchini Tanzania
yamewavutia kwani Tanzania imepiga hatua kubwa katika sekta hiyo.
Jessica alisema Serikali ya
Tanzania imeweza kuwasaidia wananchi wake kupata huduma za kibingwa bobezi
karibu na nyumbani hatua ambayo imeweza kuwarahisishia wananchi wake na
kupunguza gharama za matibabu kwa kuzifuata nje ya nchi.
"Leo tumeweza kujionea
kwa macho namna ambavyo Tanzania inafanya katika sekta ya afya, tulichokiona
hapa leo kinaonyesha kuwa maendeleo yanawezekana si kwa nadharia pekee bali kwa
vitendo”, alisema Jessica
Jessica aliongeza kuwa uzoefu
walioupata katika Taasisi hiyo utawasilishwa kwa viongozi wa sekta ya afya wa nchini
Namibia ili kusaidia mipango ya kuboresha huduma za afya na kuimarisha
ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.



.jpeg)
.jpeg)
Comments
Post a Comment