Posts

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi azungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na wazazi kuhusu umuhimu wa kufanya kipimo cha kuchunguza moyo wa mtoto aliyepo tumboni kwa wamama wajawazito ( Fetal Echoc ardiogram ). Wazazi hao walifika katika Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwaleta watoto wanaotibiwa Jkci kliniki.   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwaeleza madhara ya mafuta mwilini   wagonjwa waliokuwa wanasubiri kufanyiwa vipimo vya kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi ( Echocardiogram - ECHO)   na Umeme wa moyo ( Electrocardiogram – ECG)   wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete yapokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo (Electrocardiogram) yenye thamani ya shilingi milioni 17 kutoka kwa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo ( Electrocardiogram ) kutoka kwa Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni shilingi milioni 17.   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpulizia kisafisha mikono (hand sanitizer ) Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics)  mara baada ya kumkabidhi msaada wa mashine ya kupima umeme wa moyo ( Electrocardiogram )  kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo. Thamani ya mashine hiyo ni shilingi milioni 17. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi a...

CRDB BENKI YACHANGIA MATIBABU YA WATOTO 100 WENYE MAGONJWA YA MOYO WANAOTIBIWA JKCI

Image
Wataalam wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakitoa huduma kwa wananchi walioshiriki mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa katika taasisi hiyo leo wakati wa mbio hizo zilizofanyika katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi hundi ya Shilingi milioni 200 iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB zilizokusanywa kutoka kwa washiriki wa mbio za CRDB Marathon kwa ajili ya kuchangia matibabu ya watoto wenye magonjwa ya moyo wanaotibiwa JKCI  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi tuzo iliyotolewa leo katika viwanja vya Farasi Oyster bay Jijini Dar es Salaam na Benki ya CRDB kutambua huduma zina...

Klabu ya Mazoezi ya Xtreme Workout Bootcamp watembelea wodi ya watoto JKCI

Image
Wanachama wa klabu ya mazoezi ya Xtreme workout bootcamp wakifanya usafi katika jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo walipotembelea watoto waliolazwa katika jengo hilo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia gharama za kutengeneza kadi mbili za bima ya afya kwa watoto leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam  Wanachama wa klabu ya mazoezi ya Xtreme workout bootcamp wakifanya usafi katika jengo la watoto wenye magonjwa ya moyo walipotembelea watoto waliolazwa katika jengo hilo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto pamoja na kuchangia gharama za kutengeneza kadi mbili za bima ya afya kwa watoto leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam  Mama mwenye mtoto aliyelaza katika wodi ya watoto wenye magonjwa ya moyo Halima Selemani akipokea zawadi za mwanae kutoka kwa wanachama wa klabu ya mazoezi ya Xtreme workout bootcamp waliotembelea JKCI kwa ajili ya kufanya usafi katika jengo la watoto pamo...

Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara na kuwa na bima ya afya ambayo itawasaidia pindi watakapouguwa

Image
Wataalamu wa magonjwa wa moyo wakiangalia maendeleo ya aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rosemary Mpella akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. Lucas Lumambo Selelii aliyefanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mshipa wa damu kwenye moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Wananchi wameshauriwa kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara kwa kufanya hivyo watatambua kama wana maradhi au la na kama wana maradhi wataweza kupata huduma za matibabu kwa wakati. Pia wameombwa kuwa na bima ya afya ambazo zitawasaidia kupata matibabu pindi watakapouguwa kwani maradhi huja muda wowote, wakati wowote na mahala popote bila ya kupiga hodi. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na aliyekuwa Mbunge wa Nzega Mhe. L...

Shiriki CRDB Bank Marathon kwa ajili ya kuchangisha fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza kuhusu asilimia kubwa ya watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo kusumbuliwa na  magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari  uliofanyika leo jijini Dar es Salaam uliohusu mbio za CRDB Bank Marathon. Viongozi wa Taasisi mbalimbali ambazo zitashiriki katika mbio za CRDB Bank Marathon wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB   Abdulmajid  Nsekela mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari uliohusu mbio hizo ambazo lengo lake ni  kuchangisha fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zisizo na uwezo wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Viongozi wa Taasisi mbalimbali ambazo zitashiriki katika mbio za CRDB Bank Marathon wakiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa waandishi wa habari uliohusu mbio hizo ambazo lengo lake ni ...

WATAALAM WABOBEZI WA MOYO WAPANDIKIZA KIFAA CHA KUUSAIDIA MOYO KUFANYA KAZI VIZURI BILA KUTUMIA MTAMBO WA CATHLAB

Image
Kwa mara ya kwanza wataalamu wabobezi wa moyo na wazibuaji wa mishipa ya damu ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepandikiza kifaa cha kuusaidia moyo kufanya kazi vizuri (Pacemaker) nje ya Taasisi hiyo bila ya kutumia mtambo wa Cathlab. Mgonjwa aliyewekewa pacemaker alipata ajali iliyosababisha uti wa mgongo  kupata shida na kusababisha baadhi ya viungo vya mwili kupoteza  uwezo wa kufanya kazi ikiwemo mishipa ya damu  inayoratibu uwezo wa moyo kutengeneza mapigo yake (Sympathetic Waves System). Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaama daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Yona Gandye alisema kutoka na tatizo alilolipata mgonjwa mara baada ya kupata ajali  mapigo ya moyo yalishuka hadi kufikia 30 kwa dakika na mgonjwa kuonesha   dalili za ukosefu wa mahitaji muhimu ya mwili  yanayosambazwa na mapigo ya moyo ambayo  ni oxygen , ...