Posts
Prof Janabi: Sigara husababisha vifo tatribani milioni nane kwa mwaka duniani
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumzia madhara ya matumizi ya tumbaku na athari zake kwa wagonjwa wa moyo na wagonjwa wa UVIKO -19 wakati wa mkutano wa kutoa tathmini ya jinsi makampuni ya tumbaku yanavyoingilia sera za afya na sera za kudhibiti tumbaku ulioandaliwa na chama cha kudhibiti Tumbaku Tanzania na kufanyika katika Ukumbi wa mikutano JKCI jana jijini Dar es Salaam. Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kutoa tathimini ya jinsi makampuni ya tumbaku yanavyoingilia sera za afya na sera za kudhibiti tumbaku ulioandaliwa na Chama cha kudhibiti Tumbaku Tanzania uliofanyika jana katika Ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) uliopo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Kudhibiti Tumbaku Tanzania (TTCF) Lutgard Kagaruki akitoa matokeo mbalimbali ya tafiti walizofanya kuhusu makampuni ya tumbaku yanavyoathiri afya na kusababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza wakati wa mkutano wa kutoa tathimini ya...
319 wachunguzwa moyo Dodoma Festival
- Get link
- X
- Other Apps
Afisa muuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo zilizokuwa zinazotolewa na wataalamu wa JKCI katika tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwaja vya Chinangali park jijini Dodoma wakati akimpima kiwango cha sukari mwilini. Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekya ya Afya mara baada ya kumalizika kwa tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwanja vya Chinangali park. Tamasha hilo lilienda sambamba na zoezi la upimaji wa afya. Mkuu wa wilaya ya Dodoma Jabir Shekimweri akimkabidhi Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda cheti cha ushiriki wa tamasha la Karibu Dodoma festival lililomalizika jana katika viwanja vya Chinangali park. Mhasibu wa Taasisi ya Moyo Ja...
Pinda: Huduma za afya kibingwa zipelekwe kila Kanda
- Get link
- X
- Other Apps
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima akizungumza kuhusu umuhimu wa kusogeza huduma za matibabu ya kibingwa kwa wananchi alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kuona huduma za upimaji na matibabu ya moyo zilizokuwa zinazotolewa na wataalamu wa taasisi hiyo katika tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwanja vya Chinangali park. Kushoto ni Mkurugenzi wa JKCI Prof. Mohamed Janabi. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Geophrey Pinda ameiomba wizara ya Afya kusogeza huduma za matibabu ya kibingwa ya kuwafuata wananchi mahali walipo katika ngazi ya mikoa na kanda kwa kufanya hivyo wananchi wengi watafikiwa na huduma hizo. Pinda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kavuu alitoa ombi hilo kwa waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Doroth Gwajima katika tamasha la Karibu Dodoma festival lililofanyika katika viwaja vya Chinangali park ambalo lilikwenda sambamba na zoezi l...
Profesa Janabi: Wahudumu wa afya wawe wa kwanza kuchanja chanjo ya UVIKO – 19
- Get link
- X
- Other Apps
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi ambaye pia ni mhamasishaji wa kitaifa wa mpango wa jamii shirikishi na harakishi wa elimu na uhamasishaji wa chanjo dhidi ya UVIKO – 19 akitoa elimu ya chanjo hiyo kwa watumishi wa afya wa hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili Mirembe na wanafunzi wa chuo cha uuguzi Dodoma kilichopo chini ya hospitali hiyo. Watumishi wa afya nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchanja chanjo dhidi ya UVIKO – 19 kwani wapo katika hatari kubwa ya kupata maam b ukizi ya ugonjwa huo kupita wagonjwa wanaowahudumia ukilinganisha na watu wengine. Rai hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati akitoa elimu ya chanjo kwa watumishi wa afya wa hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili Mirembe na wanafunzi wa chuo cha uuguzi Dodoma kilichopo chi n i ya hospitali hiyo. Prof. Janabi ambaye pia ni m...
Madaktari wazawa wa JKCI kwa mara ya kwanza wapandikiza mishipa miwili ya damu katika moyo bila ya kuusimamisha moyo (Off-Pump Coronary Artery Bypass Surgery)
- Get link
- X
- Other Apps
Madaktari wazawa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa mara ya kwanza wakipandikiza mishipa miwili ya damu katika moyo bila ya kuusimamisha moyo (Off-Pump Coronary Artery Bypass Surgery) kwa mgonjwa ambaye mishipa yake mitatu ya damu ilikua imeziba na uwezo wa moyo kufanya kazi ukiwa umeshuka na kubaki asilimia 27 hivyo kumsababishia kuchoka na kushindwa kufanya kazi leo katika Taasisi hiyo Jijini Dar es Salaam
Wafanyakazi bora wa JKCI wapongezwa
- Get link
- X
- Other Apps
Mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya kwanza Joshua Ogutu akiunganisha vifaa kwa ajili ya kuwasha mashine ya kumsaidia mgonjwa kupumua (Ventilator) ikiwa ni moja ya majukumu yake ya kazi za kila siku Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwete (JKCI) Hildergurd Karau akipokea cheti kwa niaba ya Mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya pili Afisa muuguzi Mohamed Wamara kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora leo Jijini Dar es Salaam. Mfanyakazi bora wa robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2021/2022 aliyeshika nafasi ya tatu Kelvin Manyanga akipokea cheti cha mfanyakazi bora kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi hao iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.