Posts

Tanzania na China kuendeleza ushirikiano katika matibabu ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo ya kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya daktari kutoka Jamhuri ya Watu wa China Prof. Zhahg Hailong wakati wa kuwaaga madaktari watatu kutoka China waliokuwa wanafanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha kuthamini mchango wake daktari kutoka Jamhuri ya Watu wa China Sun Xufang wakati wa kuwaaga madaktari watatu kutoka China waliokuwa wanafanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi cheti cha kumshukuru kwa kazi nzuri aliyoifanya daktari kutoka Jamhuri ya Watu wa China Wang Jun wakati wa kuwaaga madaktari watatu kutoka China waliokuwa wanafanya kazi JKCI kwa kipindi cha miaka miwili hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Madaktar...

Wagonjwa 125,466 watibiwa JKCI Dar Group

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza na wafanyakazi wa JKCI hospitali ya Dar Group wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika hivi karibuni katika Hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa JKCI Hospitali ya Dar Group Dkt. Tulizo Shemu akielezea mafanikio ya Hospitali hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika hivi karibuni katika Hospitali ya JKCI Dar Group iliyopo jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi wa JKCI Hospitali ya Dar Group wakifuatilia taarifa zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge (hayupo pichani) wakati wa kikao na wafanyakazi hao kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Daktari wa JKCI Hospitali ya Dar Group Mlagwa Yango akielezea huduma zinazotolewa kwa wagonjwa wanaofika katika Hospitali hiyo wakati wa kikao cha wafanyakazi kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Hospitali hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa...

WANANCHI 761 WAPATA HUDUMA YA TIBA MKOBA YA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumalizika kwa mbio za Siha Marathon 2023 zilizofanyika hivi karibuni mkoani Kilimanjaro. Wananchi wa Siha wakijadili mambo mbalimbali huku wakisubiri kufanyiwa vipimo vya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku sita ya upimaji na matibabu ya moyo iliyomalizika hivi karibuni katika hospitali ya Wilaya ya Siha. Na: JKCI ********************************************************************************************** Watu 761 wamepata huduma ya tiba mkoba ijulikanayo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya moyo katika kambi maalum ya matibabu iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Wilaya Siha. Kambi hiyo ilifanyika kwa muda wa siku sita kuanzia tarehe 18 hadi 23/12/2023 ambapo watu w...

Aliyebadilishwa valvu ya moyo aeleza hali ilivyokuwa

Image

Dkt. Mollel: Wataalamu wa Afya tengeni muda wa kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini

Image
 Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel na wataalamu wa Taasisisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na simba mweupe walipotembelea  shamba la wanyamapori  Serval Wildlife  kwaajili ya kufanya utalii wa ndani. Wataalamu wa JKCI walikuwa    katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa    huduma za upimaji na matibabu ya moyo. Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifanya utalii wa ndani wa kuwalisha wanyama walati walipotembelea shamba la wanyamapori Serval Wildlife Siha llililopo wilayani Siha. Wataalamu wa JKCI walikuwa    katika Hospitali ya Wilaya ya Siha kwaajili ya kutoa    huduma za upimaji na matibabu ya moyo. Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizungumza na wacheza ngoma ya kimaasai wakati wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) walipotembelea shamba la wanyamapori  Serval Wild...

Balozi Polepole kushirikiana na JKCI kuboresha matibabu ya moyo

Image
Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona namna ambavyo watashirikiana katika kuboresha huduma ya matibabu ya moyo. *********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************    Balozi wa Tanzania nchini Cuba Mhe. Humphrey Polepole amesema kuwa atashirikiana na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora za matibabu ya moyo. Mhe. Balozi Polepole ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kuona namna ambavyo nchi ya Cuba inaweza kushirikiana na Tanzania katika utoaji wa huduma za matibabu ya magonjwa ya moyo. Alisema nc...

Dkt. Mollel: Wananchi wengi zaidi kufikiwa na huduma za kibingwa za matibabu ya moyo

Image
Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimkabidhi   Mkuu wa Wilaya ya Siha Mhe. Dkt. Christopher Timbuka funguo za gari moja kati ya matatu yaliyotolewa na Serikali kwa wilaya hiyo ambalo litatumika katika huduma za afya. Licha ya kukabidhi gari hilo Mhe. Dkt. Mollel alifungua kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali ya wilaya ya Siha.  Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiukabidhi uongozi wa wilaya ya Siha vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 900 ambavyo vitatumika katika Hospitali ya wilaya ya Siha. Licha ya kukabidhi vifaa hivyo Mhe. Dkt. Mollel alifungua kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa hospitali ya wilaya ya Siha. Naibu Waziri wa Afya na Mbunge wa jimbo la Siha Mhe. Dkt. Godwin Mollel akizun...