Posts

Wananchi Ilala wachangamkia fursa ya upimaji magonjwa ya moyo

Image
Wananchi wa Wilaya ya Ilala wakiendelea na huduma za vipimo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika kwa siku nne katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Gidion Mwangosi akimpa ushauri baada ya kupima mwananchi wa Ilala wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu. Afisa Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akimuuliza maswali ya ufahamu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza mwananchi aliyefika katika kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mk...

JKCI yapata tuzo katika kongamano la kisayansi nchini Kenya

Image
  Tafiti mbili kati ya tano za magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) zimechaguliwa kuwa tafiti bora na kupewa tuzo katika kongamano la kisayansi la 41 la mabingwa wa moyo nchini Kenya. Tafiti hizo mbili zilizopewa tuzo zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy) utafiti ambao umechukua miaka nane kufuatilia tatizo hilo. Akizungumza na mwandishi wa habari hii Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo alisema aliwasilisha tafiti hizo katika kongamano la kisayansi la 41 lililoandaliwa na chama cha madaktari bingwa wa moyo wa Kenya (Kenya Cardiac Society) na kufanyika mwishoni mwa wiki iliyopita. “Tafiti mbili kutoka JKCI zilichaguliwa kuingia kwenye ushindani wa tafiti bora na kupewa tuzo, tafiti hizi zilihusiana na utafiti wa ugonjwa wa moyo kutanuka kutokana na uzazi (Peripartum Cardiomyopathy)”, alisema Dkt. Pedro Dkt. Pedro ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunz...

Wananchi wa Wilaya ya Ilala wajitokeza kupima moyo

Image
Mtaalamu wa Maabara wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Mahamoud Hassan akimpima wingi wa sukari kwenye damu Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Sabina Zakaria akimpima shinikizo la damu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala Said Sidde wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanyika katika Zahanati ya Bungoni Kata ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo maalumu ya siku nne inafanywa na Hospitali ya JKCI Dar Group kwakushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa jimbo la Ilala. Naibu ...

Mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni wenye thamani zaidi ya shilingi milioni 500 wazinduliwa Hospitali ya JKCI Dar Group

Image
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu akikata utepe wakati wa uzinduzi wa mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni uliofanyika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu akikagua eneo lililowekwa mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni wakati akizundua mtambo huo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group. Mtambo huo hadi kusimikwa umegharimu shilingi milioni 526,604,116 Mhandisi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Abella Rwiguza akimuelezea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu namna mtambo wa kuzalisha hewa ya oksijeni unavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa mtambo huo leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) H...

Wanawake wa JKCI washirikiana katika matukio ya kijamii

Image
Wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha wanawake JKCI Dkt. Angela Muhozya wakimkaribisha Afisa Muuguzi mstaafu wa Taasisi hiyo Rehema Bakari wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Afisa Muuguzi Mstaafu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rehema Bakari akikata keki wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanywa na wanawake wa Taasisi hiyo jana jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti wa chama cha wanawake wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Angela Muhozya akimkabidhi zawadi ya kitenge Afisa Muuguzi mstaafu wa JKCI Rehema Bakari wakati wa hafla fupi ya kumuaga iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Chama hicho pia kimempatia Bi. Rehema zawadi ya fedha taslim Tshs. 1,300,000. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akimpa kitenge cha pole ya kuondokewa na mzazi wake mfanyakazi wa JKCI Eng. Veronica Mugendi wakati wa kikao cha wanawake wa JKCI kilichofa...

Watu 1,628 watibiwa moyo katika maonesho ya Sabasaba

Image
Katibu Mkuu Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Suleiman Aboud Jumbe akimkabidhi tuzo ya mshindi wa pili kwa utoaji wa huduma za afya na matumizi ya teknolojia katika tiba Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda jana wakati wa kufunga maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam (Sabasaba). Baadhi ya washiriki wa maonesho ya sabasaba kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifurahia baada ya kupokea tuzo ya mshindi wa pili kwa utoaji  wa huduma za afya na matumizi ya teknolojia katika tiba wakati wa kufunga maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stanley Dickson akitoa elimu ya lishe bora kwa mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma zinazotolewa wakati wa maonesho ya 48 ya kimataifa ya biashara Dar es Salaam yaliyomalizika jana katika viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara y...

JKCI yazindua kamati ya kusimamia masuala ya fedha endelevu

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati tendaji inayoshughulikia masuala endelevu ya fedha ya JKCI baada ya kuizundua leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi Mwenyekiti wa kamati tendaji inayoshughulikia masuala endelevu ya fedha ya taasisi hiyo Mr. Iddi Lema adidu rejea za majukumu ya kamati hiyo leo wakati wa uzinduzi wa kamati hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni katibu wa kamati hiyo CPA. Agness Kuhenga Na: JKCI ****************************************************************************************************************