Uchunguzi wa Afya kwenye Kazi: JKCI yawafikia Watumishi wa Serikali
Mkurugenzi wa Tiba Shirikishi wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwa sasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Salehe Mwinchete akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa watumishi wa umma wanaoshiriki Kikao kazi cha 6 cha Serikali Mtandao kinachofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC) . Wataalamu wa JKCI wanatoa huduma ya Uchunguzi na matibabu ya moyo kwenye kikao kazi hicho. Mtaalamu wa vipimo vya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Beatrice Mwakabende akimpima Mtumishi wa Umma kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi wakati wa Kikao kazi cha 6 cha Serikali Mtandao kinachofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha (AICC). Afisa Uuguzi wa Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) ambayo kwasasa inasimamiwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nadia Zuberi akimpima kipimo cha kuangalia uwiano baina ya urefu na uzito (BMI) Mtumishi wa Umma aliyehudhuria Kikao Kazi cha...