Wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo

Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Mkoa wa Geita waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa CZRH wanafanya kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikoa ya Jirani Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akimsikiliza mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka CZRH leo katika Viwanja vya Hospitali hiyo. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gerson Mpondo akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (...