Upasuaji wa kuzibua valvu za moyo kwa kutumia mtambo wa Cathlab wafanyika JKCI
Wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watu wazima wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la
Madaktari Afrika la nchini Marekani wakifanya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa
kupasua sehemu ndogo kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab kuzibua Valvu ya moyo
(Valve Intervention - Mitral Valve balloon Valvuloplasty Procedure) kwa mgonjwa
ambaye valvu yake imeziba na kushindwa kupitisha damu katika kambi maalum ya
matibabu ya moyo ya siku nne
inayoendelea katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na Khamis Mussa
Comments
Post a Comment