Wafanyakazi wa NMB Kanda ya Dar es Salaam wachangia Sh. Mil. 5 kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Mil. 5 Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa NMB Tawi la Muhimbili, Frank Makungu na kulia ni Mhasibu Mapato wa JKCI CPA. Reuben Nyiti.
Mtaalamu kutoka Mpango wa Taifa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Robinson William, akimtoa damu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, wakati wafanyakazi wa kanda hiyo wa Benki ya NMB waliposhiriki uchangiaji damu kwa ajili ya kusaidia watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu kutoka Mpango wa Taifa Damu Salama Kanda ya Mashariki, Robinson William, akimtoa damu Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya wakati wafanyakazi NMB kanda ya Mashariki waliposhiriki zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kusaidia watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam. Wafanyakazi hao walichangia Sh. Mil. 5 kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu ya watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard akizungumza wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipofika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kutoa msaada wa Sh. Mil. 5 kwa ajili ya kusaidia gharama za matibabu pamoja na kuchangia damu ambayo itatumika kwa watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moya Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya akizungumza na wafanyakazi wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, waliofika katika Taasisi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa Sh. Mil. 5 ambao utatumika kusaidia gharama za matibabu pamoja na kuchangia damu kwa watoto wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.
Comments
Post a Comment