Wananchi wa Mkoa wa Geita na mikoa ya jirani wafanyiwa uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo

Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Mkoa wa Geita waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo. Wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa CZRH wanafanya kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikoa ya Jirani

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akimsikiliza mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalum ya siku tano inayofanywa na wataalam wa afya wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka CZRH leo katika Viwanja vya Hospitali hiyo.

Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Gerson Mpondo akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo. 

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sauli Mwanyelele akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikao ya jirani inayofanywa na wataalam wa afya kutoka JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa CZRH


 Mtafiti kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) Ayoub Panja akichukua taarifa za mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato (CZRH) wakati wa kambi maalum ya siku tano ya uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wa mkoa wa Geita na mikao ya jirani inayofanywa na wataalam wa afya kutoka JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa CZRH

Picha na: JKCI

*********************************************************************************************

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)