Watoto 60 kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya siku tano iliyoanza leo jijini Dar es Salaam
Wataalamu wa upasuaji moyo na mishipa ya damu kwa
watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la
Mending Kids la nchini Marekani wakimfanyia
upasuaji wa kutengeneza valvu ya upande wa kushoto wa moyo mtoto ambaye valvu
yake ilikuwa inavuja damu. Upasuaji huo umefanyika katika kambi maalum ya siku
tano ya matibabu ya moyo iliyoanza leo JKCI ambapo watoto 60 wenye matatizo ya
moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji wa kufungua na bila
kufungua kifua.
Madaktari bingwa wa usingizi na wagonjwa mahututi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na mwenzao kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakihakikisha Valvu iliyofanyiwa marekebisho inafanya kazi vizuri kwa kutumia mashine ya Trans esophageal ECHO kabla ya kutoa moyo katika mashine ya kuusaidia moyo na mapafu kufanya kazi wakati wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo iliyoanza leo katika Taasisi hiyo iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu wa kuendesha mashine ya kuusaidia moyo na
mapafu kufanya kazi (Heart Lung Machine) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) na mwenzake kutoka Shirika la Mending Kids la nchini Marekani wakichukua
taarifa za mgonjwa anayefanyiwa upasuaji wa moyo kutoka kwenye mashine hiyo wakati
wa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyoanza leo JKCI
ambapo watoto 60 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo wanatarajia kufanyiwa upasuaji
wa kufungua na bila kufungua kifua.
Picha Khamisi Mussa
Comments
Post a Comment