watoto 70 kufanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalum ya matibabu ya siku tano iliyoanza leo tarehe 10 hadi 14/10/2022
Wataalam wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa nchini Saudi
Arabia ambao ni moja ya mradi wa Afya ulioko ndani ya Taasisi ya Msaada ya
Muntada yenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakifanya upasuaji
wa bila kufungua kifua wa kuziba tundu la moyo wa mtoto kwa kupasua sehemu
ndogo kwenye paja kwa kutumia mtambo wa Cathlab katika kambi maalum ya matibabu
ya moyo ya siku tano iliyoanza leo Jijini Dar es Salaam. Katika kambi hiyo
watoto 70 wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo, matundu na mishipa ya damu
ya moyo kutokukaa katika mpangilio wake watafanyiwa upasuaji wa moyo wa
kufungua na bila kufungua kifua
Picha na Khamis Mussa
*******************************************************************************************************
Comments
Post a Comment