JKCI yazindua mfumo wa kidijitali wa kufuatilia wagonjwa majumbani ujulikanao kama DOZEE mkoani Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuonesha Waziri wa
Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda shuka maalumu lijulikanalo
kama DOZEE wakati wa uzinduzi wa shuka hilo kwaajili ya kuwahudumia wagonjwa wa
Arusha wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu
inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimuonesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda shuka maalumu lijulikanalo kama DOZEE wakati wa uzinduzi wa shuka hilo kwaajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Arusha wakati wa kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha
Mwananchi wa Arusha
akiwa amelala katika kitanda kilichowekwa shuka maalumu lijulikanalo kama DOZEE
wakati wa uzinduzi wa shuka hilo kwaajili ya kuwahudumia wagonjwa wa Arusha
uliofanyika katika kambi maalumu ya kupima na kutibu magonjwa ya binadamu
inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Waziri wa Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya (JKCI) Dkt. Peter Kisenge na wafanyakazi wa
Taasisi hiyo tawi la Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC) mara baada ya
kutembelea hospitali hiyo iliyopo jijini Arusha
Na JKCI
**********************************************************************************************************
Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini Mhe. Paul Makonda ameipongeza Serikali ya Awamu ya
Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwekeza
teknolojia za kisasa katika sekta ya afya.
Pongezi
hizo alizitoa wakati akizindua huduma ya kuwafuata wagonjwa majumbani kwa
kutumia shuka maalumu lijulikanalo kama DOZEE wakati wa kambi maalumu ya kupima
na kutibu magonjwa ya binadamu inayofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid
uliopo jijini Arusha.
Mhe.
Makonda ambaye pia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo alisema Tanzania
ni miongoni mwa nchi zinazoendelea kupiga hatua barani Afrika katika matumizi
ya ubunifu wa kidijitali kuboresha huduma za matibabu ya moyo na kutekeleza
malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
“Matumizi
ya teknolojia katika usajili wa wagonjwa, utunzaji wa kumbukumbu za kitabibu na
ufuatiliaji wa wagonjwa wakiwa wamelazwa na baada ya matibabu kwa kutumia shuka
la DOZEE ni sehemu ya maono ya Serikali ya kujenga taifa lenye uchumi
unaotegemea maarifa, sayansi na teknolojia”, alisema Mhe. Makonda
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter
Kisenge alisema tekniolojia ya DOZEE ina uwezo wa kufuatilia viashiria muhimu
vya afya kwa mgonjwa vinavyojulikana kitaalamu kama vital signs
ikiwemo mapigo ya moyo, kiwango cha oksijeni kwenye damu na shinikizo la damu.
“Kwa
lugha rahisi DOZEE ni mfumo unaotumia kifaa maalumu kinachowekwa chini ya
godoro la mgonjwa na kufuatilia viashiria muhimu vya afya bila kulazimika
kuunganisha vifaa vingi moja kwa moja kwenye mwili wa mgonjwa”, alisema Dkt.
Kisenge
Dkt.
Kisenge alisema taarifa za mgonjwa zinazokusanywa kupitia mfumo wa DOZEE
zinaweza kumfikia daktari kwa njia ya kidijitali ikiwemo kupitia simu ya
mkononi hivyo kumwezesha kufuatilia mwenendo wa afya ya mgonjwa hata akiwa nje
ya hospitali au akiwa anaendelea na shughuli nyingine.
“Tunatumia
teknolojia hii tukiwa na malengo ya kusaidia kupunguza vifo vinavyoweza
kuzuilika hususan vinavyotokea baada ya hali ya mgonjwa kubadilika ghafla akiwa
nyumbani baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini”,
“Wagonjwa
wanaporuhusiwa kwenda nyumbani hali zao zinaweza kubadilika ghafla, Shinikizo
la damu linaweza kushuka, mapigo ya moyo yanaweza kwenda kwa kasi sana au
kiwango cha oksijeni kwenye damu kikapungua. Kupitia teknolojia hii, daktari
anaweza kupata taarifa kwa wakati na kuchukua hatua mapema kabla hali ya
mgonjwa haijawa mbaya,” alisema Dkt. Kisenge.
Huduma
hiyo ya DOZEE sasa kuanza kutumika kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Centre (ALMC).




Comments
Post a Comment