Watoto 77 wafanyiwa upasuaji wa moyo ndani ya wiki moja
Naibu Balozi wa Saud Arabia Nchini Tanzania Mhe. Abdallah Al - Harbi akiwapongeza madaktari kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia kwa ushirikiano wanaoufanya katika kutoa huduma za matibabu ya moyo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyomalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akielezea umuhimu wa ushirikiano katika kutoa huduma za afya hapa nchini wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto iliyofanywa na madakari wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Kituo cha Mfalme Salman cha Misaada ya kibinadamu kilichopo nchini Saudi Arabia na kumalizika leo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete iliyopo Jijini Dar es Salaam. Daktari bingwa wa wagonjwa waliolazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) kutoka nchini Saudi Arabia Loay Abdulsamad akieez...