Posts

Wachezaji wa klabu ya Yanga wafanyiwa vipimo vya moyo kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ya vilabu

Image
Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima jinsi moyo unavyofanya kazi mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ya vilabu Afisa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Haule akimpima urefu, uzito, na uwiano wa urefu na uzito (BMI) mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Yanga African Sport Club Clement Mzize wakati wachezaji wa timu hiyo walivyofika JKCI jana kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa ya vilabu Picha na: Khamis Mussa *******************************************************************************************************************  

JKCI yatoa elimu ya utalii tiba katika maonesho ya Sabasaba

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikweye (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima mapigo ya moyo kama yanadunda inavyotakiwa mkazi wa Dar es Salaam aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA). Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikweye (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpima kiwango cha oksijeni mwilini mtoto aliyefika katika banda la Taasisi hiyo kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa agonjwa ya  moyo wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA). Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Baraka Ndelwa akiwafundisha wanafunzi wa shule ya Sekondari Tusiime jinsi ya kujikinga na magonjwa ya moyo walipotembelea banda la hilo kwaajili ya kujifunza wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA). Wataalam wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiendelea kutoa huduma k...

Madaktari Afrika watoa msaada wa vifaa tiba vya bilioni moja

Image
Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akiwa katika picha ya pamoja na madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani alipowatembelea kabla ya kuanza kwa kambi maalum ya siku tano ya matibabu ya umeme wa moyo leo jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel akimsikiliza Daktari bingwa wa moyo na mfumo wa umeme wa moyo kutoka Shirika la Madaktari Afrika lililopo nchini Marekani David Singh alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuonana na madaktari hao kabla ya kuanza kwa kambi maalum ya matibabu ya umeme wa moyo ya siku tano inayofanyika JKCI.  Na: JKCI *********************************************************************************************************************** Shirika la Madaktari Afrika lililopo nchini Marekani limetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni moja ambavyo vitatumika katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya m...

JKCI yashiriki mbio za Figo Marathon

Image
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) anayehudumia kliniki ya VIP Odilia Njau akimpima urefu na uzito mkazi wa Dar es Salaam aliyeshiriki katika mbio za Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Janeth Mmari akimpima shinikizo la damu mkazi wa jijini Dar es Salaam aliyeshiriki katika mbio za Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mbio hizo zimefanyika leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Afisa Masoko wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Irene Mbonde akimkabidhi Mkuu wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila  kipeperushi kinachoonyesha huduma zinazotolewa na JKCI  wakati wa mbio za  Figo Marathon za kuchangia matibabu ya wagonjwa wa figo wanaotibiwa ...

Huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zatolewa Sabasaba

Image
Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Fidelice Mafumiko akimsikiliza mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabella Mkojera alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)  Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira Jamal Katundu akizungumza na mratibu wa wagonjwa wa kimataifa wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salome Mbunga alipotembelea banda la JKCI wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba)  Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Noel Majule akimwelezea mwananchi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo umuhimu wa kuchunguza afya yake wakati wa maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Honoratha Maucky akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) mwananchi aliyefika katika banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 47 ya Biash...

JKCI mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya Sabasaba

Image
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimkabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akimpongeza Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda baada ya Taasisi hiyo kuibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo. ***************************************************************************************************************** Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imeibuka mshindi wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vil...

JKCI kushirikiana na Chuo Kikuu cha New York Marekani katika mafunzo na utafiti

Image
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao wa Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman wakijadiliana namna ya kushirikiana katika masuala ya utafiti na mafunzo ya magonjwa ya moyo na kubadilishana uzoefu wa jinsi  ya kufanya tafiti hizo leo jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Idara ya Mafunzo na Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akielezea namna ambavyo idara yake imekuwa ikifanya tafiti za magonjwa ya moyo wakati wa ugeni wa wajumbe kutoka Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman walipotembelea JKCI leo kwaajili ya kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kushirikiana katika masuala ya utafiti, mafunzo na kubadilishana uzoefu katika eneo la utafiti. Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha New York Marekani Idara ya Tiba Grossman kitengo cha Afya ya Jamii Prof. Anna Bershteyn akielezea namna ambavyo chuo hicho kinafanya utafiti wa magonjwa mbalimbali ya binadamu alipofika katika  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete...