Posts

Wananchi Iringa wachangamkia fursa ya kupima moyo

Image
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Mafunzo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Pedro Pallangyo akizungumza na mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jalack Milinga akimpima kipimo cha kuangalia sukari mwilini mwananchi aliyefika katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akiwaelezea umuhimu wa lishe bora wananchi waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) kwaajili ya kupima moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH. Afisa Uuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) Diana Nyagawa akimpima ure...

Kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto

                                                       TAARIFA KWA UMMA KAMBI MAALUMU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza tutafanya kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto tarehe 20-27/04/2024. Kambi hii ya siku nane ambayo ni ya upasuaji mdogo wa moyo kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab itafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam. Tunawaomba wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo yakiwemo matundu, mishipa ya damu na valvu za moyo (PDA, ASD, VSD for device closure, na PS) wawalete katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu. Aidha tunawaomba madaktari ku...

Zaidi ya watu 11,250 wafikiwa na huduma ya tiba mkoba ya matibabu ya kibingwa ya moyo

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Eva Wakuganda akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Kigoma kuhusu kambi maalumu ya siku tatu ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na  wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Maweni . Mratibu wa Huduma za Afya Mkoa wa Kigoma Dkt.Frank Sudai  akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani humo kuhusu kambi maalumu ya siku tatu ya upimaji na matibabu ya moyo inayofanywa na  wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  –  Maweni .  Wananchi wa mkoa wa Kigoma wakisubiria kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa  –  Maweni  katika kambi maalumu ya siku tatu ya uchunguzi na mat...

Huduma za matibabu ya moyo zatolewa mkoani Iringa

Image
Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakisoma vipeperushi vinavyotoa elimu ya jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo na umuhimu wa lishe bora wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH). Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa waliojitokeza kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH).  Afisa Uuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH) Dorah Kivenule akimpima mwananchi Shinikizo la damu wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH).  Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akimpima mzunguko wa tumbo mwananchi kabla ya ku...

Wengi wafaidika na huduma za kibingwa za matibabu ya moyo

Image
Fundi sanifu wa moyo (Cardiovascular technologist) wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Jasmine Keria akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) mkazi wa Iringa aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Grace Sanga akimpima sukari kwenye damu mwananchi wa Iringa aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa IRRH. Afisa Uuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) Mary Lyimo akimpima kipimo cha kuangalia shinikizo la damu mwilini (BP) mwananchi wa Iringa aliyefika katika Hospitali hiyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya kikwete ...

UVCCM Jimbo la Ilala watoa zawadi kwa watoto wenye matatizo ya moyo

Image
Mwenyekiti wa  Umoja wa Vijana  wa Chama Cha Mapinduzi  (UVCCM) jimbo la Ilala Boaz Stanton akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Ustawi wa Jamii wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Asha Salum zawadi mbalimbali kwa ajili ya watoto waliolazwa  katika Taasisi hiyo pamoja na walezi wao wanaowauguza.  Mwenyekiti wa   Umoja wa Vijana   wa Chama Cha Mapinduzi   (UVCCM) kata ya Mchikichini Anna Msala   akimkabidhi zawadi Monica Mayunga ambaye   mtoto wake anatibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati viongozi hao wa UVCCM jimbo la   Ilala walipotembelea JKCI leo kwa ajili ya kutoa zawadi kwa watoto waliolazwa   katika Taasisi hiyo pamoja na walezi wao wanaowauguza. Mwenyekiti wa   Umoja wa Vijana   wa Chama Cha Mapinduzi   (UVCCM) kata ya   Upanga Magharibi   Salma Ishaq akimkabidhi zawadi   Ester   Yohana kwa ajili ya mtoto wake aliyelazwa   katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete ...

Wafanyakazi wa JKCI washiriki Iftari ya pamoja

Image
Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akizungumza na wafanyakazi wa JKCI  wakati wa Iftari ya pamoja iliyoandaliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akiwaongoza wafanyakazi wa taasisi hiyo kuchukuwa chakula wakati wa Iftari ya pamoja iliyoandaliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakichukuwa  chakula wakati wa Iftari ya pamoja iliyoandaliwa na Taasisi hiyo hivi karibuni jijini Dar es Salaam.