Kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto
TAARIFA KWA UMMA
KAMBI MAALUMU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza tutafanya kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto tarehe 20-27/04/2024.
Kambi hii ya siku nane ambayo ni ya upasuaji mdogo wa moyo kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab itafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
Tunawaomba wazazi wenye watoto wanaosumbuliwa na matatizo ya moyo yakiwemo matundu, mishipa ya damu na valvu za moyo (PDA, ASD, VSD for device closure, na PS) wawalete katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu.
Aidha
tunawaomba madaktari kutoka Hospitali zote nchini kuwapa rufaa watoto wenye
matatizo hayo ili waje JKCI kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.
Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0744-479506 Dkt. Jimmy France na 0788-308999 Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Imetolewa na:
Genofeva
Matemu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na
Mawasiliano
17/04/2024
Comments
Post a Comment