Kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo mkoani Iringa


Afisa Lishe waTaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Maria Samlongo na Mtaalamu wa Tiba - Viungo Jenes Blasio wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba (BRRH) wakitoa elimu ya lishe bora na umuhimu wa kufanya mazoezi kwa wananchi waliofika katika hospitali hiyo mwezi wa tatu mwaka huu kwa ajili ya kupata huduma za upimaji na matibabu ya moyo. 
 *********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH) watatoa huduma za tiba mkoba zijulikanazo kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa na  mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 15/04/2024  hadi tarehe 19/04/2024 kuanzia saa mbili kamili asubuhi mpaka saa 10 kamili jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH).

Kutakuwa na wataalamu wa lishe ambao watatoa elimu ya lishe bora ambayo itawapa wananchi uelewa na  kufuata mtindo bora wa maisha utakaowasaidia kuepukana na magonjwa ya moyo ambayo ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza na yanaweza kuepukika kwa kufuata ushauri wa kitaalamu.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapohapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi yetu.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0767054453 Dkt. Alfred Mwakalebela  Mkurugenzi wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa  na 0657926892 Dkt.Faith Kundy .

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.




Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari