Kambi maalumu ya upimaji na matibabu ya moyo mkoani Kigoma

 Daktari waTaasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sigfrid Shayo akimpima mgonjwa shinikizo la damu (BP) wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya upimaji na matibabu ya moyo iliyofanyika mwezi wa kwanza mwaka huu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Tabora – KITETE.

***********************************************************************************************************************************************************************************

Wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Maweni (Maweni RRH) iliyopo Mkoani Kigoma watatoa huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa jina la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma na  mikoa ya jirani.

Upimaji huu utafanyika kwa watoto na watu wazima tarehe 16-18/04/2024 saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Maweni.

Watakaogundulika kuwa na matatizo ya moyo watafanyiwa uchunguzi zaidi na kupatiwa matibabu hapo hapo au kupewa rufaa ya kuja kutibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Tunawaomba wananchi mjitokeze kwa wingi kupima afya zenu kujua kama mna matatizo ya moyo ili kuanza matibabu mapema kwa atakayegundulika kuwa mgonjwa.

Kwa taarifa zaidi wasiliana kwa simu namba 0654344254,0753528030 na 0800112021 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa – Maweni.

“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari