Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud aipongeza JKCI
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimweleza Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo wakati Rais huyo alipotembelea Taasisi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa na Taasisi hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akiangalia video fupi inayoonesha huduma zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.

Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akizungumza na viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati alipotembelea taasisi hiyo leo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuona huduma za matibabu ya moyo zinazotolewa.
**********************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Rais wa Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud amewapongeza wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa huduma nzuri wanayoitoa ya kuokoa maisha ya watu wenye matatizo ya moyo.
Mhe. Rais Hassan Sheikh Mohamud alizitoa pongezi hizo leo jijini Dar es Salaam
alipotembelea Taasisi hiyo (JKCI) kwaajili
ya kuona huduma za matibabu ya moyo
zinazotolewa.
Akiwa katika Taasisi hiyo Mhe. Rais Mahamud alitembelea
maeneo mbalimbali ya JKCI ikiwa ni
pamoja na mtambo wa Cathlab ambayo ni maabara inayotumia mionzi maalumu
kwaajili ya kufanya uchunguzi na matibabu ya moyo.
Akizungumzia kuhusu ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema JKCI ni moja ya
Taasisi inayoongoza katika nchi za Afrika Mashariki na kati katika kutoa huduma
za kibingwa za matibabu ya moyo.
Dkt. Kisenge alisema Rais Mohamud alitembelea Taasisi hiyo
kwaajili ya kuona namna ambavyo nchi ya
Somalia itawapeleka wagonjwa wa moyo JKCI kupata tiba ya matibabu ya moyo.
“Nchi ya Somalia inawapeleka wagonjwa wengi wa moyo kwenda kutibiwa katika nchi za India,
Ulaya na Marekani wakati huduma hii
inapatikana nchini Tanzania, na ukiangalia nchi hizi ziko karibu hivyo basi
itakuwa ni rahisi kwao kuwaleta wagonjwa kuja kutibiwa hapa kwetu”.
“Kuja kwa wagonjwa hawa kutaisaidia nchi yetu kukua kiuchumi
kwani pesa zitakazopatikana zitawafikia watu wengi ikiwemo wamiliki wa hoteli
ambako wagonjwa watalala pamoja na wafanyabiashara watakaowauzia vyakula na
mahitaji mengine”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt. Kisenge
alimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuimarisha mahusiano na nchi
za nje ndiyo maana watu wengi wanakuja kuwekeza hapa nchi hata Taasisi hiyo
imekuwa ikiwapokea wageni mbalimbali
kutoka nchi za nje.
Akiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Mhe. Rais Hassan Sheikh Mohamud pamoja na ujumbe wake aliambata na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
Comments
Post a Comment