Viongozi watembelea banda la JKCI maonesho ya Osha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dickson Minja alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.

Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma akipimwa shinikizo la damu na Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Odilia Njau alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.


Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hildergard Karau akimpima sukari kwenye damu mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.

Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Benson Bisare akimwelezea mwananchi uhusiano kati ya urefu na uzito mara baada ya kupima uzito wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Highridge iliyopo jijini Arusha wakimsikiliza daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dickson Minja alipokuwa akiwafundisha jinsi moyo unavyofanya kazi wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.

Na: JKCI

*********************************************************************************************************

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepongezwa kwa kusogeza huduma karibu na wananchi na kuwafanyia uchunguzi na matibabu ya moyo wananchi wa mkoa wa Arusha.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Deogratius Ndejembi alipotembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa kambi maalumu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services katika maonesho ya kimataifa ya usalama na afya mahali pa kazi yanayofanyika viwanja vya General tyre jijini Arusha.

Mhe. Ndejembi alisema JKCI imekuwa ikifanya vizuri katika kutoa huduma za matibabu ya moyo nchini na kuwa kimbilio kwa wananchi wengi wenye magonjwa ya moyo.

“Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya, JKCI naijua vizuri kutokana na huduma zake za kipekee inazozitoa za matibabu ya moyo hapa nchini”, alisema Mhe. Ndejembi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la JKCI Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma alishukuru kwa kupatiwa huduma za uchunguzi wa afya na ushauri kutoka kwa wataalamu wa afya.

“Nawashukuru wataalamu wa afya wa JKCI kwa kunipa nafasi ya kupima afya yangu lakini hamkuishia hapo bali mmeweza pia kunipa elimu kuhusu mfumo bora wa maisha”, alisema Dkt. Mduma

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule ya msingi Highridge Adam Washokera alisema alipofika katika banda hilo na kupatiwa huduma aliona kuna fursa ya kuwaleta wanafunzi wa shule yake kujifunza kuhusu moyo kwani ni vitu ambavyo wanafunzi wanajifunza darasani.

“Baada yakufika katika banda hili na kupatiwa huduma niliona fursa ya kuwaleta wanafunzi wa darasa la nne na la saba kujifunza kuhusu moyo kutoka kwa daktari bingwa wa moyo kwani daktari anaujua moyo vizuri hivyo watoto wamepata elimu kwa vitendo”, alisema Adam

Adam alisema baadhi ya wanafunzi wamekuwa na ndoto ya kuwa madaktari hivyo wakisogezwa karibu na watu wa ndoto zao wanapata motisha zaidi kusoma na kufikia ndoto zao.

Naye mwananfunzi wa darasa la saba shule ya msingi Higridge Joshua Proches alisema amefurahi kufika katika banda la JKCI kupata elimu na kujua nini kinachosababisha mtu kupata magonjwa ya moyo.

“Nimekuwa nikisikia watu wanaumwa moyo lakini sikuwa najua moyo unaumwa vipi na nini kinasababisha moyo kuumwa lakini baada ya kupata elimu kutoka kwa daktari nimejua”, alisema Joshua

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari