Watoto 40 wafanyiwa upasuaji wa moyo kwa muda wa siku tano


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa mradi wa Little Heart uliopo ndani ya shirika la Muntada Aid lenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza.

Meneja wa miradi wa Shirika la Muntada Aid Kabir Miah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  kwa kushirikiana na wenzao wa shirika hilo kupitia mradi wa Little Heart.


Mkuu wa Kitengo cha magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja akizingumza na  waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa chanjo kwa watoto wakati wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao wa mradi wa Little Heart uliopo ndani ya shirika la Muntada Aid lenye makao makuu yake mjini London nchini Uingereza.

*********************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Watoto 40 tafanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi maalumu ya matibabu iliyofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikia na wenzao wa Shirika la Muntada Aid la nchini Uingereza kupitia mradi wa Little Heart. 

Gharama ya upasuaji kwa mtoto mmoja ni Sh Milioni 15 ndani ya nchi ambapo nje ya nchi ni Sh milioni 30.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge alisema upasuaji huo umeanza Aprili 20 ,2024 ambapo tayari watoto 24 wamekwishafanyiwa upasuaji huku lengo likiwa ni kufikia watoto 40.

"Tangu tarehe 20 taasisi yetu ilipata wageni kutoka Uingereza  walikuwa wanakuja wakati taasisi ilikuwa hali ya chini kwa upasuaji wa moyo hawa wametupa historia kubwa wamesaidia kufundisha madaktari wetu na watoto zaidi ya 500 wamefanyiwa upasuaji.

Dkt. Kisenge alisema wataalamu hao ni muungano wa madaktari mbalimbali kutoka Canada,Uholanzi,Misri na Uingereza na wamependa kuja hapo kutokana na miundombinu iliyoboreshwa na serikali na rasilimali watu.

"Serikali hivi karibuni imetoa bilioni tano kusomesha madaktari katika ubingwa bobezi hawa wakija wanataka kuona miundombinu mizuri na hawa pia wamekuja na vifaa tiba vya gharama ya Sh bilioni 1.5 wamekuja navyo na wametuachia kuwasaidia wenzetu”, alisema Dkt.Kisenge.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Magonjwa ya Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja alisema katika kila watoto 1,000  wanaozaliwa watoto nane mpaka 10 wanazaliwa na matatizo ya moyo.

"Hapa tunaona wagonjwa hadi 50 kwa siku wanaopewa rufaa kutoka sehemu mbalimbali za mikoani,rufaa na Muhimbili, wenzetu hawa  wanapokuja na vifaa tunafaida tunapata ujuzi mpya kila siku teknolojia inabadilika na maarifa yanaongezeka”, alisema Dkt. Kubhoja.

Meneja wa miradi wa Shirika la Muntada Aid,Kabir Miah alisema wanafanya kazi Afrika katika nchi mbalimbali na hasa sehemu ya afya ambapo mradi huo unaokoa maisha ya watoto wanaoteseka na magonjwa ya moyo.

Alisema wameokoa maisha ya watoto 3,000 katika nchi 10 na wamekuja hapa mara nyingi kufanya upasuaji kwa zaidi ya watoto 500.

"Sasa hapa kuna miundombinu ya kutosha na tunafuraha kufanya kazi hapa tunawashukuru kuhakikisha mradi huu unafanikiwa”, alisema Miah.

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari