JKCI yashinda tuzo za heshima za uhusiano na mawasiliano
Mkurugenzi wa Idara ya Habari – MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda tuzo ya ushindi wa kwanza katika kutoa elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo (Public Services Campaign) iliyotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yessaya Mwakifulefule akimkabidhi Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda tuzo ya mshindi wa pili wa kutoa huduma kwa jamii ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo (Corporate Social Responsibility) iliyotolewa na Chama cha Maafisa Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST).
Taasisi ya moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) imeshinda tuzo mbili za heshima za uhusiano na mawasiliano
katika kutoa elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya moyo (Public Services Campaign) na
kutoa huduma kwa jamii ya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo (Corporate Social Responsibility)
zilizotolewa na Chama cha Maafisa
Uhusiano na Mawasiliano Tanzania (PRST).
Tuzo hizo zimetolewa jana jijini
Dar es Salaam katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa St.Peter’s na kuhudhuriwa
na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca
Mahundi.
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imeshinda tuzo hizo
kupitia huduma za tiba mkoba zinazojulikana kwa jina
la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inazozifanya kwa kufanya upimaji na matibabu ya magonjwa ya moyo kwa kuwafuata wananchi mahali walipo. Hadi sasa Taasisi hii imeshaifikia
mikoa 13 ya Tanzania bara na visiwani na kufanya upimaji kwa watu 11,254.
Upimaji huo unakwenda sambamba na utoaji wa elimu kwa umma
kuhusu magonjwa yasiyo ya kuambukiza yakiwemo ya moyo na matumizi sahihi ya
dawa za moyo, kuwajengea uwezo wataalamu wa afya wa jinsi ya kuwatambua
wagonjwa wa moyo na kufanya utafiti wa magonjwa ya moyo.
Ushindi huo pia umetokana
na mchango mkubwa unaotolewa na Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano katika
kuuhabarisha umma kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Taasisi pamoja na
kutoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa wananchi.
“Afya ya Moyo Wako ni Jukumu Letu”.
Comments
Post a Comment