Huduma za matibabu ya moyo zatolewa mkoani Iringa

Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakisoma vipeperushi vinavyotoa elimu ya jinsi ya kuepukana na magonjwa ya moyo na umuhimu wa lishe bora wakati wa kambi maalumu ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH).

Afisa lishe wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Husna Faraji akitoa elimu ya lishe kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa waliojitokeza kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH). 

Afisa Uuguzi kutoka Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH) Dorah Kivenule akimpima mwananchi Shinikizo la damu wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayoendelea katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa (IRRH). 

Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Loveness Mfanga akimpima mzunguko wa tumbo mwananchi kabla ya kufanyiwa vipimo vya moyo katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH).

Wananchi wa Mkoa wa Iringa wakijisajiri kwaajili ya kupatiwa huduma katika kambi maalumu ya siku tano ya matibabu ya moyo inayofanywa na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa (IRRH).

Picha na: Khamis Mussa

************************************************************************************************************

 

Comments

Popular posts from this blog

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yapata tuzo ya taasisi ambayo imetoa mchango wa kipekee kiuchumi na kijamii katika kuleta matokeo makubwa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024

Maabara ya JKCI yapata ithibati ya kimataifa (ISO 15189:2012)