Posts

Dkt. Kisenge: Wanamichezo na Wasanii pimeni afya za mioyo yenu

Image
  Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiograph - ECHO) mchezaji wa mpira wa miguu. ********************************************************************************************************** Wanamichezo na wasanii wametakiwa kufanya uchunguzi wa afya za mioyo yao mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa hayo ambayo yanaweza kuwasababishia kupata tatizo la shambulio la moyo au kifo cha ghafla. Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge wakati akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Dkt. Kisenge alisema kupima afya ya moyo ni muhimu kwani mtu anaweza kuwa na matatizo hayo bila ya kuwa na dalili hivyo kuwataka wanamichezo kutoanza michezo ghafla kwani mwili unaweza kutengeneza mabadiliko ambayo yanaweza kuleta madhara ikiwemo kupata s...

JKCI yawafikia washirika wa KKKT Wazo hill

Image
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akimsikiliza mwananchi aliyefika kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill jijini Dar es Salaam. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Fatma Suedy akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyefika kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tatu ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba inayofanywa na JKCI katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Wazo Hill jijini Dar es Salaam. Fundi sanifu wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hospitali ya Dar Group Devotha Mapunda akimpima kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiography – ECG) mwananchi aliyefika kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa...

Wataalamu wa Rediolojia wa JKCI kuendelea kulinda afya za wagonjwa

Image
Wataalamu wanaotoa huduma za rediolojia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakikata keki wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba. Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Shirikishi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akizungumza na wataalamu wa rediolojia wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba. Daktari bingwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) George Longopa akielezea namna huduma za upasuaji mdogo wa moyo unavyotumia mionzi wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba. Mkuu wa Kitengo cha Rediolojia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Praygod Lekasio akiwapongeza wataalamu wa rediolojia kwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa wakati wa kuadhimisha siku ya rediolojia duniani inayofanyika kila ifikapo tarehe 8 mwezi Novemba. Baadhi ya wataalamu wa rediolojia wa Taasisi ya Moyo Jakaya...

JKCI yatoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari

Image
Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wahariri   unaofanyika jijini Dar es Salaam. Daktari Bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samuel Rweyemamu akitoa elimu ya magonjwa ya moyo kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wa mwaka wa wahariri unaofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa JKCI Anna Nkinda. Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akiishukuru Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kuwatuma wataalamu wake kwenda kutoa elimu pamoja na kufanya upimaji wa magonjwa ya moyo  kwa Wahariri wa vyombo vya habari waliohudhuria mkutano wao wa mwaka unaofanyika jijini Dar es Salaam. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akizungumza na Wahariri wa vyom...

Shirika la Save a Childs Heart laipa JKCI kifaa cha kupima moyo chenye thamani ya shilingi Milioni 200

Image
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea kifaa kinachotumika kupima moyo (Transesophageal Echocardiography (TEE) probe) kwa watoto chenye thamani ya shilingi milioni 200 kilichotolewa na wataalamu wa afya kutoka Shirika la Save a Childs Heart lililopo nchini Israel wakati wa harambee ya kuchangia matibabu ya watoto iliyofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana iliyopo jijini Dar es Salaam. Jumla ya shilingi bilioni 4.1 zilikusanywa kwaajili ya matibabu ya moyo kwa watoto. Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka shirika la Save a Childs Heart lililopo nchini Israel wakimfanyia mtoto upasuaji  wa kuziba tundu lililopo kwenye kupitia mtambo wa cathlab wakati wa kambi maalumu iliyomalizika hivi karibuni. Jumla ya watoto 19 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa moyo. Picha na: JKCI  ********************************************************************************************************************

Afanyiwa upasuaji wa kuziba tobo lililokuwa kwenye chemba ya moyo

Image
Wataalamu wa upasuaji mkubwa wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani wakimfanyia upasuaji wa kurekebisha mshipa mkubwa wa damu (Aorta) mgonjwa ambaye mshipa wake mkubwa umetanuka wakati wa kambi maalumu ya siku tano iliyofanyika katika Taasisi hiyo na kumalizika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. *************************************************************************************************** Kijana mwenye umri wa miaka 19 amefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo kuziba tobo lililokuwa kwenye chemba ya chini ya moyo upande wa kushoto hivyo kupelekea damu kuzunguka nje ya moyo (LV Pseudo aneurysm). Upasuaji huo umefanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwakushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Cardio Start International la nchini Marekani. Akizungumza na mwandishi wa habari hii daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jaka...

JKCI yawanoa wataalamu wa afya jinsi ya kufanya kipimo cha ECHO

Image
Daktari wa watoto kutoka Hospitali ya KCMC Lightness Chuwa akiwaongoza madaktari wenzake kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) wakati wa mafunzo ya siku tano kwa wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali yanayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwakushirikiana na Pediatric Association of Tanzania na German Tropical Pediatrics (GTP). Mkufunzi kutoka Utrecht nchini Netherlands Dkt. Martijn Slieker akiwafundisha wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi namna ya kuyatambua magonjwa ya moyo kwa watoto wakati wa mafunzo ya siku tano ya kufanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography – ECHO) yanayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Pediatric Association of Tanzania na German Tropical Pediatrics (GTP). Wataalamu wa afya kutoka Hospitali mbalimbali nchini wakifanya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography - ECHO) ...