Wapimwa viashiria vya magonjwa ya moyo kwenye Tamasha la EFM Jogging
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akimkabidhi cheti cha ushiriki wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwenye Tamasha la EFM jogging Afisa Uuguzi wa JKCI Oliver Marandu wakati wa Tamasha hilo lenye kauli mbiu Tokomeza magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika leo katika viwanja vya Dry Morocco jijini Dar es Salaam. EFM wameandaa Tamasha hilo kwa ajili ya kuchangia damu kwa wagonjwa wanaotibiwa JKCI na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Maafisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwapima shinikizo la damu wadau wa jogging walioshiriki kwenye Tamasha la EFM Jogging lenye kauli mbiu Tokomeza magonjwa yasiyoambukiza lililofanyika leo katika viwanja vya Dry Morocco jijini Dar es Salaam. EFM wameandaa Tamasha hilo kwa ajili ya kuchangia damu kwa wagonjwa wanaotibiwa JKCI na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khairoon Mohamed akimuelezea madhara yanayoweza kusababishwa na mtindo m...