Wachangia damu kuokoa maisha ya watoto wanaofanyiwa upasuaji wa moyo
Mjumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Utalii Tiba Abdulmalik Mollel akipimwa wingi wa damu ili aweze kuchangia damu ambayo itatumika kwa watoto watakaofanyiwa upasuaji wakati wa kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na wataalam wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza.Kambi hiyo itafanyika tarehe 12/05/2023 hadi 19/05/2023 jijini Dar es Salaam.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Adv. Haruni Matagane akichangia damu ambayo itatumika kwa watoto watakaofanyiwa upasuaji wakati wa kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza.Kambi hiyo itafanyika tarehe 12/05/2023 hadi 19/05/2023 jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Salma Jumanne akimtoa damu mwananchi aliyejitokeza kuchangia damu ambayo itatumika kwa watoto watakaofanyiwa upasuaji wa moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza. Kambi hiyo itafanyika tarehe 12/05/2023 hadi 19/05/2023 jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama Rajabu Kwesa akimtoa damu mwananchi aliyejitokeza kuchangia damu ambayo itatumika kwa watoto watakaofanyiwa upasuaji wakati wa kambi maalum ya matibabu itakayofanywa na wataalam wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza. Kambi hiyo itafanyika tarehe 12/05/2023 hadi 19/05/2023 jijini Dar es Salaam.
*********************************************************************************************************************************************************************************************************
Chupa 44 za damu
zimekusanywa katika zoezi la kuchangia damu kwaajili ya watoto watakaofanyiwa upasuaji wakati wa
kambi maalum ya upasuaji itakayofanywa na
wataalam wa Taasisi ya Moyo ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na
wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la Muntada Aid lenye makao
yake makuu mjini London nchini Uingereza.
Kambi hiyo itafanyika tarehe 12/05/2023 hadi 19/05/2023 jijini Dar
es Salaam.
Akizungumzia zoezi hilo la kuchangia
damu Daktari bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Godwin Sharau alisema uhitaji wa damu katika upasuaji wa moyo
kwa watoto ni mkubwa kwani mtoto mmoja anaweza kutumia chupa za damu mbili
mpaka nne wakati wa upasuaji.
“Upasuaji wa moyo unahitaji damu
nyingi sana kwa sababu baadhi ya damu hutumika katika mashine inayosambaza damu
kwa mgonjwa wakati wa upasuaji na damu nyingine uandaliwa kwa ajili ya dharura
pale ambapo damu itahitajika”, alisema Dkt. Godwin.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa
Taasisi inayojihusisha na huduma za kijamii ikiwemo na kuchangia damu JAI Saad
Salim alisema kuchangia damu ni moja ya utaratibu wa kikundi hicho kwani wanafahamu
ya kwamba damu uhai na uhitajika kwa wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji.
“Huu ni utaratibu wa kikundi chetu
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya wengine, kwa hapa JKCI hii ni mara yetu ya
pili kuchangia damu, mara ya kwanza tulichangia damu mwaka 2015 ambapo kupitia
Taasisi yetu uniti 35 za damu zilipatikana”.
Akitoa wito kwa jamii kuwa na
utaratibu wa kuchangia damu Saad Salim alisema jamii inatakiwa kuona umuhimu wa
kujitokeza kuchangia damu pale huduma hiyo inapohitajika mahospitalini kwani
kuokoa maisha ya mgonjwa anayehitaji damu ni thawabu.
“Jamii itambue ya kwamba mahitaji ya
damu ni makubwa hivyo inatakiwa kuweka utaratibu wa kuchangia damu katika
mahospitali yetu kwani unapochangia damu inakwenda kuwasaidia wananchi wengine
ambao nao wanatamani kuwa na afya kama sisi tulivyo”, alisisitiza Salim.
Naye Afisa uhamasishaji Kanda ya
Mashariki kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salamu Mary Meshy alisema muitikio wa
wananchi kuchangia damu umekuwa mkubwa kwa kiasi chake lakini jamii bado
inapaswa kutambua ya kwamba damu haijawahi kutosha hivyo waendelee kuchangia
ili kuweza kuokoa maisha ya wengine.
“Watu wengi wameguswa na kufika hapa
JKCI kwa ajili ya kuchangia damu ila bado uhitaji wa damu ni mkubwa, anayepaswa
kuchangia damu kwa mwanamke asiwe mjamzito wala anayenyonyesha na asiwe na
magonjwa yoyote hasa yale ya kurithi”, alisisitiza Mary Meshy.
Akifafanua namna ambavyo ameguswa
kuchangia damu mwanafunzi wa chuo cha Paradigms Institute kilichopo Kimara
jijini Dar Es Salaam Denis Mziba alisema wanachuo wenzake kutoka chuo hicho
wameona umuhimu wa kushiriki zoezi la kuchangia damu kuwasaidia watoto
wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.
“Nimewiwa mimi na wanafunzi wenzangu kuchangia
damu ili kuweza kufanikisha matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa hapa JKCI na
tunaahidi tutaendelea kufanya hivi kila wakati”, alisema Denis.
Comments
Post a Comment