Watoto 334 wafanyiwa uchunguzi na upasuaji wa moyo katika kambi ya matibabu inayoendelea JKCI


 Madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo  kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la  Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakifanya upasuaji wa kuziba tundu la moyo wa mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika Taasisi hiyo.


Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la  Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza wakizima tundu la moyo wa mtoto wakati wa kambi maalum ya siku tano ya upasuaji wa moyo inayofanyika katika Taasisi hiyo. 

**************************************************************************************************************************************************************************************************

Watoto 334 wenye matatizo ya matundu kwenye moyo,  matatizo ya mishipa ya damu na Valve za moyo  wamefanyiwa uchunguzi na upasuaji katika kambi maalum ya ya siku tano ya matibabu ya moyo kwa watoto inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKC).

Kambi ilianza tarehe 12/05/2023 na inatarajia kumalizika tarehe 19/05/2023 inafanywa na wataalamu wa magonjwa ya moyo ya watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka mradi wa Little Heart wa Shirika la  Muntada Aid lenye makao yake makuu mjini London nchini Uingereza.

Kwa muda wa siku mbili tangu kambi hiyo ianze watoto 307 wamefanyiwa uchunguzi wa moyo ambapo kati yao watoto 19 wamefanyiwa upasuaji kwa njia ya tundu dogo ambao unafanyika kwa kutumia mtambo wa Cathlab na watoto nane wamefanyiwa upasuaji mkubwa wa moyo wa kufungua kifua.


 

Comments

Popular posts from this blog

Wateja wa CRDB kutibiwa JKCI kwa punguzo la asilimia 50%

Wanawake wa JKCI SACCOS wanaongoza kwa kumiliki hisa

JKCI, MOI NA MNH waitwa Comoro kutoa huduma za matibabu ya kibingwa