JKCI yasimamia mkutano wa kimataifa wa moyo


Madaktari bingwa wa moyo wawili kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamepata nafasi ya kushiriki katika mkutano wa Kimataifa wa EuroPCR nchini Paris kama wakaguzi wa vipindi vilivyokuwa vikiendeshwa katika Mkutano huo.

Mkutano huo wa kimataifa unaofanyika kila mwaka nchini humo kuhusu upasuaji wa moyo kwa kutumia tundu dogo mwaka huu umefanyika kuanzia tarehe 15 hadi 20 Mei na kuudhuriwa na madaktari bingwa wa moyo kutoka nchi mbalimbali ambapo Tanzania iliwakilishwa na madaktari wawili wa JKCI

Akizungumzia mkutano huo Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Khuzeima Khanbhai alisema katika mkutano huo moja ya mafunzo yaliyotolewa yalikuwa kuhusu interventional cardiology

“Mimi pamoja na mwenzangu Dkt. Emmanuel Epafra tulipewa nafasi ya kutathmini na kuwa wakaguzi wa vipindi vilivyokuwa vikiendelea wakati wa mkutano wa EuroPCR, hii inaonyesha kuwa dunia inatuamini na kuamini huduma tunazozitoa hapa JKCI”, alisema Dkt. Khuzeima

*****************************************************************************************************************

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari