Manyara kuwatibu wagonjwa elfu 11 wenye shinikizo la juu la damu kila mwaka


Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) Dkt. Yesige Mutajwaa akikata utepe kuashiria maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu huku pembeni yake daktari bingwa wa moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akimpima shinikizo la damu Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Wizara ya Afya Dkt. Anzibert Rugakingira wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa leo katika Mkoa wa Manyara 

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) Dkt. Yesige Mutajwaa akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pima shinikizo lako la damu kwa usahihi, lidhibiti ili uishi maisha marefu”.

Mratibu wa magonjwa yasiyoambukiza Wizara ya Afya Dkt. Anzibert Rugakingira akielezea namna ambavyo tatizo la shinikizo la damu linaongezeka nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pima shinikizo lako la damu kwa usahihi, lidhibiti ili uishi maisha marefu”.

Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo akielezea namna ambavyo JKCI imekuwa ikiwafikia wagonjwa wa shinikizo la damu katika mikoa mbalimbali wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pima shinikizo lako la damu kwa usahihi, lidhibiti ili uishi maisha marefu”. 

Baadhi ya wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) na wananchi wa Manyara wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pima shinikizo lako la damu kwa usahihi, lidhibiti ili uishi maisha marefu”.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara (MRRH) Dkt. Yesige Mutajwaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wataalam wa afya kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete baada ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara. Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Pima shinikizo lako la damu kwa usahihi, lidhibiti ili uishi maisha marefu”.

Na: JKCI

***********************************************************************************************************************

Wagonjwa elfu 11 wenye tatizo la shinikizo la juu la damu hupata matibabu ya ugonjwa huo kila mwaka katika vituo vya afya vilivyopo Mkoa wa Manyara.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara Dkt. Yesige Mutajwaa wakati wa maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu yaliyofanyika kitaifa leo Mkoani Manyara.

Dkt. Yesige ambaye pia daktari bingwa wa magonjwa ya ndani alisema idadi hiyo sio idadi kamili ya watu wenye shinikizo la juu la damu kwani hao elfu 11 ni idadi ya wale tu wanaopata matibabu katika Mkoa huo.

“Tangu mwaka 2018 hadi 2022 mwelekeo wa shinikizo la juu la damu kwa wananchi wa Manyara unaonyesha kuongezeka, mwaka 2018 wananchi wote walioudhuria vituo vya kutolea huduma za afya asilimia 0.9 walikutwa na shinikizo la juu la damu ambalo kila mwaka limekuwa likiongezeka hadi mwaka 2022 wagonjwa wa shikikizo la juu la damu walioudhuria vituo vya afya Manyara kufikia asilimia 1.4”, alisema Dkt. Yesige

Aidha Dkt. Yesige ameishukuru Wizara ya Afya kwa kukubali na kuuchagua mkoa wa Manyara kuwa sehemu ya maadhimisho ya siku ya shinikizo la juu la damu kitaifa kwani kupitia maadhimisho hayo kunatoa hamasa kwa wananchi wa Manyara kuona umuhimu wa kupima shinikizo la juu la damu mara kwa mara.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Pedro Pallangyo alisema JKCI ilianzisha kambi maalum za matibabu ya moyo lengo likiwa kusogeza huduma karibu na wananchi, kujengeana uwezo watumishi wa afya, pamoja na kuielimisha jamii juu ya magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt. Pedro alisema magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la juu la damu yameongezeka katika jamii hivyo ni wakati muafaka kama wadau wa afya kupigia kelele kuipa hamasa jamii kuhusu uelewa wa magonjwa hayo ili kwa pamoja jamii iweze kujikinga.

“Kwa kipindi cha mwaka mmoja Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete imewafikia wananchi zaidi ya elfu 8 katika mikoa ya Arusha, Geita, Mtwara, Lindi, Zanzibar, Iringa, Dodoma, Dar es Salaam, Pwani, na Manyara ambapo watu hao tulipowafanyia vipimo wengi tuliwakuta na shinikizo la juu la damu”,

“Wakati wa kambi hizi maalum tumekuwa tukifanya utafiti na kubaini ya kuwa wagonjwa wanne kati ya 10 tunaowaona usumbuliwa na tatizo la shinikizo la juu la damu”, alisema Dkt. Pedro

Kwa upande wa huduma zinazotolewa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Dkt. Pedro aliendelea kusema kila wagonjwa saba kati ya 10 wanaofika JKCI kwa ajili ya matibabu ukutwa na tatizo la shinikizo la juu la damu.

Naye Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza Wizara ya Afya Dkt. Anzibert Rugakingira alisema Wizara ya afya inalo jukumu la kulinda afya za watanzania hivyo ipo mstari wa mbele kuhakikisha wananchi wanajua namba zao za shinikizo la juu la damu, kujitambua na kupatiwa matibabu mapema.

Dkt. Rugakingira alisema nimuhimu kila mtu akawa na utaratibu ya kupima shinikizo la juu la damu angalau mara mbili kwa mwaka ili pale mtu anapokuwa na tatizo hilo aweze kupata matibabu kwa haraka kupunguza athari anazoweza kupata kama hatatibiwa mapema.

Dkt. Rugakingira alisema Wizara ya Afya inao mpango wa taifa wa kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la juu la damu, mpango huo ulianzishwa baada ya kuwepo na ongezeko kubwa la magonjwa hayo hapa nchini.

“Kwa muda wa kipindi cha miaka mitano utafiti umefanyika ambapo 2017 wagonjwa wa shinikizo la juu la damu walioudhuria vituo vya afya walikuwa laki sita na elfu themanini na nane, 2022 wagonjwa hao waliongezeka hadi kufikia milioni moja na laki nne, wagonjwa hawa ni wale tu wanaoudhuria kliniki naamini wapo wagonjwa wengi ambao upoteza maisha yao bila ya kufika Hospitali kupata huduma” alisema Dkt. Rugakingira

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

Wataalamu wa JKCI kufanya upasuaji wa moyo nchini Zambia

JKCI na AICC Hospitali kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo katika kikao kazi cha wenyeviti na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma

JKCI yamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kuwapa magari