Posts

Showing posts from September, 2025

JKCI yawahimiza wagonjwa matumizi sahihi ya dawa

Image
Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Benitho Ng’ingo akitoa elimu ya matumizi  sahihi ya dawa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo ikiwa ni ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani inayofanyika  tarehe 25 Septemba. Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rweyemamu Peter akiangalia dawa zinazotumiwa na mgonjwa anayetibiwa katika taasisi hiyo wakati akitoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani inayofanyika  tarehe 25 Septemba. Mkuu wa Idara ya Famasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Wellu Kaali akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafamasia wa Taasisi hiyo mara baada ya kumaliza kutoa elimu ya matumizi  sahihi ya dawa kwa wagonjwa wanaotibiwa katika taasisi hiyo  ikiwa ni ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani inayofanyika  tarehe 25 Septemba. Na JKCI ******************************************************************************************...

RMO Geita aipongeza JKCI kwa kutoa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo katika maonesho ya madini

Image
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita (RMO) Dkt. Omary Sukari akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) alipotembelea banda la taasisi hiyo leo lililopo katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini Geita kwaajili ya kuona huduma za upimaji na matibabu ya moyo zinazotolewa na wataalamu hao. Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita (RMO) Dkt. Omary Sukari akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kiwkete (JKCI) lililopo katika Maonesho ya Nane ya Kitaifa ya Teknolojiaya Madini yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan Geita kwaajili ya kuona huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa. Afisa Masoko wa  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Agnes Mndasha akimweleza Mkemia Uchenjuaji wa  dhahabu wa Chama cha Wachimbaji wa Madini Mkoa wa Geita (GEREMA)  John Ngeda  huduma zinazotolewa na Taasisi hiyo  wakati wa Maonesho ya Nane ya Kitaifa...

JKCI yazindua mfumo wa kidigitali wa miadi ya wagonjwa

Image
Afisa Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alamin Msangi akimuelekeza mgonjwa namna ya kuchukua token katika kioski baada ya mgonjwa kufunya miadi ya kumuona daktari kupitia simu janja.  Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Fiona Kavishe akionesha tovuti yenye mfumo wa kidigitali wa miadi mtandao. Afisa Tehama wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alamin Msangi akifuatilia namna ambavyo ndugu wa mgonjwa aliyelazwa JKCI anavyochukua token katika kioski kabla ya ndugu huyo kuingia kumuona mgonjwa. Na JKCI ********************************************************************************************************* Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imeanzisha mifumo miwili ya kisasa ya kuweka miadi kwa ajili ya kumuona daktari na mfumo wa namna ndugu wa mgonjwa anavyoweza kumtembelea mgonjwa aliyelazwa hospitalini. Mifumo hiyo inapatikana kupitia tovuti rasmi ya taasisi hiyo (www.jkci.or.tz) ambapo wagonjwa sasa wanaweza kuweka mi...

JKCI yatoa elimu ya Shinikizo la Juu la Damu katika maonesho ya madini G...

Image

Wananchi wapata fursa ya vipimo vya moyo katika maonesho ya madini Geita

Image
 Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Henry Mayala akimpima kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi mkazi wa Geita aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo zinazotolewa katika maonesho ya nane ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika kwenye Viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan   vilivyopo mjini Geita. Afisa Utafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Zabela Mkojera akichukua taarifa za mkazi wa Geita aliyefika katika banda la Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa maonesho ya nane ya kitaifa ya teknolojia ya madini yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Dkt. Samia Suluhu Hassan vilivyopo  mjini Geita. ***************************************************************************************************************************************************************************...

JKCI yagusa mioyo ya wanachama 125 wa TAWCA kupitia upimaji wa afya Jijini Arusha

Image
 Mwenyekiti wa Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) CPA. Mary Mabiti akimkabidhi  jana Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Ashura Ally  tuzo ya shukrani ya utoaji wa huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanachama wa chama hicho waliohudhuria mkutano wa TAWCA unaofanyika jijini Arusha. Katika mkutano huo JKCI ilitoa bila malipo huduma ya upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanachama 125. Mkuu wa Kitengo cha Fedha na Uhasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Ashura Ally akigawa vipeperushi vya kutoa elimu ya magonjwa ya moyo jana kwa wanachama wa Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) waliofika katika banda la JKCI kwaajili ya kupata huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo inayotolewa katika mkutano wa TAWCA jijini Arusha. Afisa Lishe wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Neema Matemba akitoa elimu ya lishe bora kwa mwanachama wa Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) aliyeshiriki mkutano wa ch...

Ujue Mfumo wa Mihadi ya kumuona Daktari na Mfumo wa kutembelea wagonjwa ...

Image

Kambi maalumu ya matibabu ya magonjwa ya mishipa ya damu kifuani kutanuk...

Image

Wanawake waaswa kulinda mioyo yao, kuepuka sukari na chumvi kupita kiasi

Image
Wahasibu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Ashura Ally na Edna Sanga wakifuatilia mada ya wakifuatilia mada ya    kumbukumbu gani umeiacha katika eneo lako la kazi kutokana na matendo yako mazuri uliyoyafanya iliyokuwa inatolewa katika mkutano wa Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) unaofanyika jijini Arusha. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Idrisa Ndende akimpima kiwango cha sukari kwenye damu Mhasibu aliyefika katika banda la taasisi hiyo kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa    mkutano wa Chama cha Wahasibu Wanawake Tanzania (TAWCA) unaofanyika jijini Arusha. Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA. Agnes Kuhenga na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo  Engerasia Kifai  wa taasisi hiyo  wakifuatilia mada ya  kumbukumbu gani umeiacha katika eneo lako la kazi kutokana na matendo yako mazuri uliyoyafanya iliyokuwa inatolewa  katika m...

BAPS Charity yatoa milioni 250 JKCI , Jamii yahimizwa kuokoa maisha ya w...

Image

BAPS Charity yatoa milioni 250 JKCI , Jamii yahimizwa kuokoa maisha ya watoto wenye matatizo ya moyo

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimkabidhi tuzo ya shukrani Mratibu wa BAPS Charity Tanzania Kapil Dave kutokana kujitoa kwao kuchangia fedha za matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi hiyo na jumuia ya BAPS Charity Tanzania mara baada ya    kukabidhiwa    hundi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kusaidia matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wanaotibiwa katika taasisi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimshukuru Mratibu wa BAPS Charity Tanzani  Kapil Dave mara baada ya kupokea hundi ya shilingi milioni 250 kwaajili ya kusaidia matibabu ya moyo kwa watoto wanaotoka katika familia zenye uwezo mdogo kiuchumi wa...

Wanamichezo wapewa wito wa kupima moyo kabla ya kufanya mazoezi

Image
Wachezaji wa mpira wa pete wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili  (MOI) wakishindana wakati wa bonanza la wafanyakazi la  kuhitimisha sherehe za miaka kumi  tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika  uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam. Wachezaji wa mpira wa  meza  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakicheza mchezo huo wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi  tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika  uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.  Wachezaji wa mchezo wa  pool table  wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishindana wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi  tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika  uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.  Wachezaji wa mchezo wa draft wa Taasisi ya Moyo Jakay...

Watoto 28 wafanyiwa upasuaji wa moyo, Serikali yaokoa milioni 270

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akikabidhi tuzo ya shukrani kiongozi wa timu ya watalaamu kutoka  King Salman Humanitarian Aid and Relief Center  nchini Saudi Arabia Aijohara Hamza  wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanyika JKCI.  Taasisi hiyo iliishukuru King Salman Humanitarian Aid and Relief Center kutokana na ushirikiano walionao wa kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya na matibabu ya moyo kwa watoto. Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima akimkabidhi zawadi mratibu wa  kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto kutoka King Salman Humanitarian Aid and Relief Center Alharthi Hamazah Abdulaziz wakati wa hafla fupi ya kufunga kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto iliyofanyika JKCI. Watoto 28 walifanyiwa upasuaji wa moyo katika kambi hiyo. Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwet...

JKCI yapewa jukumu kuu: Kuinua huduma za moyo barani Afrika

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule wakati mkutano na waandishi wa habari jana mjini Lusaka kuhusu kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH). Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH) Dkt. Chabwela Shumba wakati mkutano na waandishi wa habari jana mjini Lusaka kuhusu kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH). Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew Edward Mkingule akizungumza na waandishi wa habari jana mjini L...