JKCI yapewa jukumu kuu: Kuinua huduma za moyo barani Afrika
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe.
Luteni Generali Mathew Edward Mkingule wakati mkutano na waandishi wa habari
jana mjini Lusaka kuhusu kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na
wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa
Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akimpatia zawadi Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo
Zambia (NHH) Dkt. Chabwela Shumba wakati mkutano na waandishi wa habari jana
mjini Lusaka kuhusu kambi ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na
wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa
Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH).
Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Luteni Generali Mathew
Edward Mkingule akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Lusaka wakati wa
kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika
la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo
Zambia (NHH).
Mkurugenzi Mtendani wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Lusaka wakati
wa kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa
Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Okoa Moyo wa Mtoto
(SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH).
Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela akielezea namna wanavyoshirikiana na
madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH) kuwachunguza watoto wenye
magonjwa ya moyo wakati na mkutano na waandishi wa habari jana mjini Lusaka
kuhusu kambi maalumu ya upasuaji wa moyo kwa watoto inayoafanyika katika
Hospitali ya NHH iliyopo Lusaka nchini Zambia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Dkt. Peter Kisenge akizungumza na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo
Zambia (NHH) Dkt. Chabwela Shumba alipotembelea chumba cha uangalizi maalumu
(ICU) wakati wa kambi maalumu ya siku sita ya upasuaji wa moyo kwa watoto
inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la
Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia
(NHH).
Na JKCI
****************************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepewa wito wa kutumia utaalamu wake wa kibingwa kuendeleza hospitali mbalimbali barani Afrika zinazotoa huduma za matibabu ya moyo, hatua itakayosaidia kupunguza utegemezi wa bara hilo kupata huduma za matibabu nje ya Afrika na kuimarisha uwezo wa ndani wa kuhudumia wagonjwa.
Rai
hiyo imetolewa jana jijini Lusaka na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe.
Luteni Generali Mathew Edward Mkingule wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu kambi maalumu ya upasuaji wa
moyo kwa watoto inayofanywa na wataalamu wa JKCI kwa kushirikiana na Shirika la Save a Child’s Heart (SACH) la
nchini Israel na Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH).
Mhe.
Luteni Generali Mkingule alisema Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na
Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH) ni wakati wao sasa kushirikiana na
kugawana ujuzi walionao kwa maslahi ya nchi zao na Afrika kwa ujumla.
“Afrika
tunayoitaka ni ile ya mshikamano na ushirikiano, tusishindane bali
tushirikishane na kubadilishana uzoefu, ujuzi na umahiri wetu kwa ajili ya
ustawi wa watu wetu na maendeleo ya Afrika kwa ujumla”, alisema Mhe. Luteni
General Mkingule
Aidha
Mhe. Luteni General Mkingule alisema Serikali ya nchi hizo mbili inatambua na
kuthamini kwa dhati msaada wanaopata kutoka nje ya nchi hususan kutoka Shirila
la Okoa Moyo wa Mtoto (SACH) la nchini Israel kwani watoto hawana mipaka
haijalishi wapo Afrika hivyo ni vizuri wakasaidiwa kwa pamoja na kuokoa maisha
yao.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt.
Peter Kisenge alisema JKCI na NHH wamesaini makubaliano mwaka 2023 kwa ajili ya
kutoa huduma za kibingwa bobezi za matibabu ya moyo kwa watoto na watu wazima,
kutoa mafunzo kwa wataalamu wa afya na kufanya kambi maalumu za upasuaji wa
moyo angalau mara mbili kwa mwaka.
“Tangu
kusainiwa kwa makubaliano hayo JKCI imeshatoa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia
wagonjwa wa dharura na mahututi kwa wauguzi 14 kutoka Hospitali ya Taifa ya
Moyo ya Zambia, huku wanne wakiendelea na mafunzo hayo sasa”.
“Tumeshafanya
kambi maalumu za upasuaji wa moyo kwa watoto nne katika hospitali hii kwa
kushirikiana na SACH na wadau wengine wa kimataifa, na kwa sasa timu yetu ipo
hapa kwaajili ya kambi maalumu ya tano. Takriban wananchi wa Zambia 100
wamepata huduma kupitia ushirikiano huu, ambapo kati yao asilimia 43
walifanyiwa upasuaji wa moyo”, alisema Dkt. Kisenge.
Dkt.
Kisenge alisema kwa kipindi cha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake JKCI imekuwa
miongoni mwa Taasisi inayotoa huduma bingwa na bobezi za matibabu ya moyo
Afrika Mashariki na Kusini mwa Jangwa la Sahara hivyo inatamani kuona Taasisi
nyingine zinazotoa huduma hiyo hususani za umma zinapata mafanikio ambayo
taasisi hiyo imepata.
Naye
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Moyo Zambia (NHH) Dkt. Chabwela Shumba
alisema JKCI na SACH ni Taasisi mbili za kipekee zilizoamua kuungana kwa pamoja
kuokoa maisha ya watoto wenye magonjwa ya moyo waliopo nchini Zambia.
Dkt.
Shumba alisema katika kambi hiyo wataalamu hao wanafanya upasuaji wa moyo wa
kisasa kwa watoto ambao wataalamu wa Hospitali hiyo wasingeweza kufanya hivyo
ingepelekea watoto hao kupelekwa nje ya Zambia kwaajili ya matibabu.
“Katika
kambi hii tumewafanyia uchunguzi watoto zaidi ya 30 ambapo watoto 10
watafanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua na watoto 20 watafanyiwa
upasuaji wa moyo kwa njia ya tundu dogo kupitia mtambo wa Cathlab, alisema Dkt.
Shumba.
Comments
Post a Comment