Wanamichezo wapewa wito wa kupima moyo kabla ya kufanya mazoezi
.jpg)
Wachezaji wa mpira wa pete wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) wakishindana wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.
Wachezaji wa mpira wa meza wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakicheza mchezo huo wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.
Wachezaji wa mchezo wa pool table wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishindana wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.
Wachezaji wa mchezo wa draft wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili wakishindana wakati wa bonanza la wafanyakazi la kuhitimisha sherehe za miaka kumi tangu kuanzishwa kwa JKCI lililofanyika katika uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam.
********************************************************************************************************************************************
Wanamichezo nchini
wamepewa wito wa kufanya vipimo vya moyo kabla ya kuanza mazoezi au michezo ili
kubaini iwapo kuna matatizo katika mishipa ya moyo au valvu jambo linaloweza
kuokoa maisha yao.
Akizungumza mwishoni
mwa wiki kwenye Bonanza lililohusisha michezo mbalimbali ikiwemo baiskeli,
mpira wa miguu na netiboli Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Peter Kisenge alisema baadhi ya
wanamichezo hupoteza maisha ghafla kutokana na matatizo ya moyo, hususan misuli
na valvu.
“Tunawahimiza
wanamichezo kupima moyo wao kabla ya michezo, ili kudhibiti hatari ya kupata
mshtuko wa moyo. Wananchi pia wajitokeze kwenye hospitali mbalimbali kufahamu
hali zao za kiafya”, alisema Dkt. Kisenge.
Aliongeza kuwa
kujizoeza kufanya mazoezi kwa wastani wa dakika 30 kila siku kunasaidia kutoa
jasho mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukiza hususan ya
moyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bonanza
hilo Dkt. Evarist Nyawawa alisema michezo iliyofanyika ilishirikisha
taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI),
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) na Hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH).
“Michezo ni
sehemu ya ulinzi wa afya na mwendelezo wa matibabu. Tulishindana na timu kutoka
taasisi hizi na washindi wamepewa zawadi”, alisema Dkt. Nyawawa ambaye pia ni Daktari
bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI).
Naye Kapteni wa timu ya
netiboli ya JKCI, Mariamu
Maarufu alisema timu yao ilishinda dhidi ya MOI kwa kupata
mipira 19 dhidi ya 13 na kuongeza kuwa ushindi huo umetokana na maandalizi
makali na mazoezi ya mara kwa mara.
Kapteni
wa timu ya mpira wa miguu ya MNH Hemed Mohamed alisema
michezo inaimarisha afya na kuleta ari kazini, huku akisisitiza umuhimu wa kufanya
mazoezi ya kawaida kwa kila mfanyakazi.
“Michezo si burudani tu, bali ni
sehemu ya kujenga afya ya moyo na kudumisha ari kazini”, aliongeza.
Bonanza hilo lilifanyika katika uwanja wa APC Hotel & Conference Centre, Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya JKCI ambapo kabla ya bonanza hilo shughuli mbalimbali zilifanyika ikiwa ni pamoja na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wanafunzi, uzinduzi wa kamati ya kupandikiza moyo na mdahalo wa wazi wa kutoa elimu ya utalii tiba kwa wananchi.
Comments
Post a Comment