Kampuni ya Huduma za Kifedha ya ASA Microfinance kwa kushirikiana na Benki ya CRDB zatoa baiskeli 30 za wagonjwa JKCI.
Mkuu wa Idara ya Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Salma Wibonela akimuelezea Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Huduma za Kifedha ya ASA Microfinance Muhammad Shah Newaj namna ambavyo wagonjwa wanahudumiwa alipotembelea Taasisi hiyo kwaajili ya kutoa baiskeli za wagonjwa 30 kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kuwasaidia wagonjwa wanaotibiwa JKCI.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Huduma za Kifedha ya ASA Microfinance Muhammad Shah Newaj akizungumza na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Angela Muhozya mara baada ya kukabidhi baiskeli za wagonjwa 30 zilizotolewa na kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki ya CRDB kwaajili ya kuhudumia wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Upasuaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Dkt. Angela Muhozya na Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi wa JKCI Robert Mallya
wakiwakabidhi wakuu wa sehemu baiskeli za wagonjwa zilizotolewa na Kampuni ya
Huduma za Kifedha ya ASA Microfinance kwa kushirikiana na Benki ya CRDB
kwaajili ya kuhudumia wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi hiyo iliyopo jijini
Dar es Salaam.
Picha na JKCI
********************************************************************************************************************
Kampuni
ya Huduma za Kifedha ya
ASA Microfinance kwakushirikiana na Benki ya CRDB zatoa baiskeli 30 za wagonjwa
kwa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kusaidia wagonjwa wanaotibiwa katika
Taasisi hiyo.
Akizungumza
wakati wa kupokea viti hivyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Idara ya Uuguzi
wa JKCI Robert Mallya alisema baiskeli hizo zitasaidia katika kurahisisha
mzunguko wa wagonjwa wanaoingia na kutoka JKCI.
“Tunawashukuru
sana Kampuni ya Huduma
za Kifedha ya ASA Microfinance na Benki ya CRDB
kwa kuona umuhimu wa kuwajali wagonjwa wetu hivyo kuamua kutuletea baiskeli
hizo 30”, alisema Mallya
Mallya
alisema JKCI ina wagonjwa wengi ambao wanahitaji kuzungushwa na baiskeli ili
kufika katika maeneo ya kupata huduma hivyo viti mwendo hivyo vitasaidia
kurahisisha huduma.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kampuni ya Huduma
za Kifedha ya ASA Microfinance Muhammad Shah Newaj alisema mbali na kutoa huduma za fedha pia
wamejikita katika kusaidia jamii kwa kutoa vifaa tiba ili kupunguza baadhi ya
changamoto zinazo ikabili sekta ya afya.
“Huu
ni mwanzo katika kusaidia wagonjwa wa moyo ambao wanahitaji mizunguko ya kwenda
katika maeneo tofauti kupata huduma na vipimo, tutaendelea kuwafikia na kuwapa
mahitaji tofauti”, alisema Muhammad
Mohammad
alisema kampuni ya Huduma za Kifedha ya ASA iliona mwaka huu irejeshe kwa jamii
faida inayopata kwa kutoa baiskeli hizo kwa wagonjwa wa moyo wanaotibiwa JKCI.
Naye
Meneja Mwandamizi uwekezaji kwa jamii CRDB Benki Foundation Ninael Munuo alisema
lengo la ushirikiano huo na kampuni ya ASA ni kuleta matumaini kwa wagonjwa kwa
kuwapatia mahitaji muhimu wanayohitaji wanapokuwa hospitali.
“Kupitia
mbio za nyika zinazofanwa na Benki ya CRDB tumekuwa tukiwapa kipaumbele watoto
wenye magonjwa ya moyo wanaotibwa JKCI hivyo tukaona sasa tushirikiane na ASA
katika kuleta matumaini kwa wagonjwa wa JKCI wanaohitaji baiskeli kwenda sehemu
tofauti wakati wa matibabu”
Tasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikishirikiana na Taasisi mbalimbali zikiwemo
za fedha katika kuboresha huduma bingwa bobezi za magonjwa ya moyo nchini.
Comments
Post a Comment