JKCI yawahimiza wagonjwa matumizi sahihi ya dawa
Mfamasia wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Benitho Ng’ingo akitoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wagonjwa wanaotibiwa
katika Taasisi hiyo ikiwa ni ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani
inayofanyika tarehe 25 Septemba.
Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rweyemamu Peter akiangalia dawa zinazotumiwa na mgonjwa anayetibiwa katika taasisi hiyo wakati akitoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani inayofanyika tarehe 25 Septemba.
Na JKCI
********************************************************************************************************************
Wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wamehimizwa kuhusu matimizi sahihi ya dawa ili kujinga na madhara yanayoweza kutokea endapo watatumia dawa zao vibaya.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mfamasia wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Rweyemamu Peter wakati akitoa elimu ya matumizi sahihi ya dawa kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Wafamasia Duniani inayofanyika tarehe 25 Septemba.
Rweyemamu alisema wagonjwa wanapaswa kujua namna bora ya kutumia dawa pamoja na kuzingatia masaa ya kumeza dawa kwa utaratibu maalumu uliowekwa na watalaamu wa afya.
“Ni muhimu kwa wagonjwa wetu kuzingatia utumiaji na utunzaji wa dawa kwa usahihi ili waweze kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kupoteza maisha ama kupata ulemavu”, alisema Rweyemamu.
Rweyemamu alisema wagonjwa wanaopata madhara mbalimbali kutokana na dawa wanatakiwa kutoa taarifa mapema kwa wafamasia eneo walilichukua dawa ama mfamasia yeyoye aliye karibu naye ili waweza kushauriwa cha kufanya na wakati mwingine kubadilishiwa dawa ili kulinda afya zao.
Nao baadhi ya ndugu wa wagonjwa wanaopatiwa huduma JKCI walishukuru kwa elimu waliyoipata kuhusu matumizi sahihi ya dawa na namna ya kuhifadhi dawa na kusisitiza elimu hiyo kuendelea kutolewa mara kwa mara ili kuwakumbusha wagonjwa na wanaowahudumia.
“Nimefurahi kupata elimu hii hapa JKCI kwani ni hospitali chache zinazotoa elimu ya matumizi sahihi ya dama, mimi sikujua kama kuna baadhi ya dawa zikishafunguliwa kwa matumizi zinatakiwa kutumika kwa siku 28 tu na baada ya hapo hazitakiwi tena kutumika” alisema Dorothea Masusa mkazi wa Dar es Salaam.
Jumanne Ramadhani mkazi wa Geita alisema kutokana na changamoto alizokuwanazo mtoto wake ilikuwa ni muhimu kupata elimu hiyo ili asije akakosea kumpatia dawa na kumletea changamoto nyingine.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kupata elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa, kwakweli nimefaidika sana na nitahakikisha namlinda mtoto wangu kwa kufuata ushauri wa daktari na mfamasia katika kutumia dawa”, alisema Ramadhani.
Siku ya wafamasia duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 25
Septemba ili kuikumbusha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa na umuhimu wa
wafamasia katika kusimamia utoaji wa dawa sahihi kwa wagonjwa.
Comments
Post a Comment