JKCI kuanzisha kampuni tanzu kuimarisha tiba utalii nchini
Mwenyekiti
Msaidizi wa Kamati ya Maandalizi ya mpango mkakati wa watu wa Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) Iddi Lemah akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi hiyo
wakati wa kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa tatu wa JKCI kwa wafanyakazi kilichofanyika
jana katika ukumbi wa JKCI iliopo jijini Dar es Salaam.
Mshauri
wa maandalizi ya mpango mkakati wa watu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Ivan Tarimo akielezea vitu vilivyoanishwa katika mpango mkakati huo wakati wa
kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa tatu wa JKCI kwa wafanyakazi kilichofanyika
jana katika ukumbi wa Taasisi hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akielezea
namna ambavyo mpango mkakati wa tatu wa JKCI utakavyoboresha huduma wakati wa
kikao cha kuwasilisha mpango mkakati huo kwa wafanyakazi kilichofanyika jana katika
ukumbi wa Taasisi hiyo iliopo jijini Dar es Salaam.
Daktari
bingwa wa upasuaji wa moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Msoka
akichangia mada wakati wa kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa tatu wa Taasisi hiyo
kilichofanyika jana katika ukumbi wa JKCI iliopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia mada
zilizokuwa zikiendelea wakati wa kikao cha kuwasilisha mpango mkakati wa tatu
wa Taasisi hiyo kilichofanyika jana katika ukumbi wa JKCI iliyopo jijini Dar es
Salaam.
Na JKCI
***************************************************************************************************
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) imepanga kuanzisha kampuni tanzu itakayojikita
katika shughuli za tiba utalii, kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba na huduma
nyingine za kimkakati kwa lengo la kuongeza ufanisi wa huduma zinazotolewa na
Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Hayo
yameelezwa na Mwenyekiti Msaidizi wa Kamati ya Maandalizi ya Mpango Mkakati wa
tatu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wa mwaka 2026/27 mpaka 2030/2031 Iddi
Lemah wakati wa kuwasilisha mpango mkakati huo kwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo
jana jijini Dar es Salaam.
Lemah
alisema mpango mkakati huo umeandaliwa na kuwashirikisha kwa wafanyakazi wa
Taasisi hiyo ili kuhakikisha kila mmoja anaelewa malengo ya Taasisi na
kushiriki katika utekelezaji wake.
“Mpango
mkakati huu utawanufaisha wafanyakazi kwa sababu ndio njia ya kujipima yale
malengo ambayo tumejiwekea tunayafikia katika kipindi cha miaka mitano na namna
gani tutashirikiana kuendeleza huduma hizi bingwa bobezi za moyo”, alisema
Lemah.
Lemah
alisema moja ya maeneo mapya yaliyowekwa katika mpango mkakati huo ni pamoja na
kuanzishwa kwa kampuni tanzu itakayosaidia kuongeza ufanisi wa taasisi katika
maeneo mbalimbali ya kimkakati.
“Kampuni
tanzu hiyo itashughulika na tiba utalii, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na
kushirikiana na kampuni mbalimbali za nje ya nchi katika upatikanaji wa vifaa
tiba”, alisema Lemah.
Kwa
upande wake Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Tunzo
Lundgreen alisema mpango mkakati huo umewekwa malengo ambayo yanayotekelezeka
hivyo ni muhimu wafanyakazi wakashirikiana kwa pamoja kufanya kazi kwa ufanisi.
“Mpango
mkakati wa mwaka 2026/27 mpaka 2030/2031 umehusisha mambo yote muhimu ambayo
Taasisi inafanya kwa kuzingatia masuala uendelevu ya upanuzi wa Taasisi, utalii
tiba, masuala ya fedha pamoja na utawala bora”,
“Kama
Taasisi itasimamia vizuri rasilimali zake na kuendeleza ubunifu mbalimbali
uliowekwa kwenye mpango mkakati huu itaongeza kipato na kuimarisha huduma zake katika
kipindi cha miaka mitano ijayo”, alisema Tunzo.
Mpango
mkakati huo unatarajiwa kuwa dira ya maendeleo ya JKCI katika kipindi cha miaka
mitano ijayo kwa kuimarisha huduma za matibabu ya moyo, kuendeleza tiba utalii
na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali zilizopo.



.jpeg)


Comments
Post a Comment