Siku mbili tu zaidi ya watu 200 watibiwa moyo kambi maalum Shinyanga

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akimsikiliza mkazi wa Shinyanga aliyefika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Shinyanga (SRRH) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo wakati wa kambi maalumu ya siku tano ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanyika mkoani Shinyanga. Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akigawa vipeperushi vya elimu ya magonjwa ya moyo kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga waliofika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga (SRRH) kwaajili ya kupata huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya moyo. Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga wakisoma vipeperushi vya elimu ya magonjwa ya moyo na taarifa mbalimbali za Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa kambi maalumu ya Tiba Mkoba ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Services inayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyang...