Wazazi wahimizwa kuwatibu watoto ugonjwa wa mafindofindo kuwaepusha na magonjwa ya valvu za moyo
Daktkari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Alex Benjamini akishirikina na wenzake kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani kumfanyia mgonjwa upasuaji wa kufungua kifua kurekebisha mshipa mkubwa wa damu (Aorta) wakati wa kambi maalumu ya siku nne iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo. Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu kutoka Shirika la Madaktari Afrika la nchini Marekani na mwenzake kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakivuna mshipa wa damu katika mguu wa mgonjwa kwaajili ya kuupandikiza katika moyo wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya upasuaji wa moyo iliyomalizika jana katika Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam Wataalamu wa afya wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimfanyia kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Cardiography – ECHO) mgonjwa ambaye mshipa wake mkubwa wa damu (Aorta) umetanuka wakati wa kambi maalumu ya siku nne ya matibabu hayo iliyomalizika jana k...