Kliniki ya JKCI iliyopo SABASABA yaanza kutoa huduma kwa wananchi
Baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa
ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Nyanjura Nyaruga akimpima kiwango cha sukari kwenye damu mwananchi aliyetembelea banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Happy
Malunde akiwaelezea huduma zinazotolewa katika chumba cha upasuaji wa wananchi waliotembelea
banda la Taasisi hiyo wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar
es Salaam (SABASABA) yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
vilivyopo barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Nyanjura Nyaruga akimpima shinikizo la damu mwananchi aliyetembelea banda la
JKCI wakati wa maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (SABASABA)
yanayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo
barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Na JKCI
*********************************************************************************************
Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) kupitia kliniki yake iliyopo katika maonesho ya 50 ya Kimataifa
ya Biashara (SABASABA) yaanza kutoa huduma za uchunguzi na matibabu ya magonjwa
ya moyo kwa wananchi wanaotembelea katika maonesho hayo.
Kupitia kliniki hiyo
wananchi wanapimwa shinikizo la damu, sukari kwenye damu, mafuta kwenye damu, kipimo
cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echocardiography), na kipimo cha kuangali
mfumo wa umeme wa moyo (Electrocardiogram - ECG).
Vipimo vingine
vinavyofanyika katika banda hilo ni vipimo vya maabara pamoja na kutoa chanjo
ya homa ya ini. Aidha wananchi wanaotembelea banda la JKCI wanapata fursa ya
kupata ushauri kuhusu lishe bora kutoka kwa wataalamu waliobobea katika lishe.
Ili kuboresha afya za
wananchi JKCI imepanga kutumia maonesho hayo kama sehemu ya kuongeza jitihada dhidi
ya kinga ya magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya moyo kutokana na magonjwa hayo
kuongezeka na kupunguza nguvu kazi ya taifa.
Sambamba na kauli mbiu
ya maonesho hayo JKCI imejipanga kuwa fahari ya Tanzania kupitia maonesho ya 50
ya SABASABA kwa kutoa huduma bora kwa kila mwananchi atakayetembelea banda
hilo.
.jpeg)
.JPG.jpeg)



Comments
Post a Comment