JKCI yang'ara mkutano wa kimataifa wa PEN-PLUS (ICPPA 2026), yaonesha teknolojia inayotumia katika matibabu ya moyo.
.jpeg)
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama akimuelezea mshiriki wa mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Kikanda PEN-PLUS (ICPPA 2026) kutoka nchini Zambia James Titus huduma zinazotolewa na taasisi hiyo alipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano huo uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na kumalizika jana jijini Dar es salaam
Afisa Uuguzi wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Karen Ngobei akiwaeleza washiriki wa
mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Kikanda PEN-PLUS (ICPPA 2026) kuhusu huduma
zinazotolewa na taasisi hiyo walipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano huo
uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na
kumalizika jana jijini Dar es salaam.
Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama akimuelezea mshiriki wa mkutano wa tatu wa Kimataifa wa Kikanda PEN-PLUS (ICPPA 2026) kutoka Boston nchini Marekani Gehe Bakhman huduma zinazotolewa na taasisi hiyo alipotembelea banda la JKCI wakati wa mkutano huo uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na kumalizika jana jijini Dar es salaam.
***********************************************************************************************************
Washiriki wa Mkutano
mkuu wa tatu wa Kimataifa wa kikanda PEN-PLUS (ICPPA 2026) wavutiwa na huduma
zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walipotembelea banda la Taasisi hiyo washiriki hao walisema JKCI ni miongoni mwa Taasisi za Afya nchini Tanzania ambayo imekuwa ikipambana kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya magonjwa ya moyo.
James Titus kutoka nchini Zambia alisema JKCI imekuwa mstari wa mbele katika kutoa matibabu, kinga na elimu kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ndani na nje ya mipaka ya Tanzania ikiwemo nchini Zambia.
“Taasisi hii imekuwa mfano wa kuigwa katika nchi yetu kutokana na mikakati inayoifanya kuhakikisha kuwa utalamu walionao unawekezwa pia kwa wataalamu wetu ili kwapamoja tuweze kudhibiti magonjwa ya moyo ambayo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza”, alisema Titus
Titus alisema
kupitia mkutano huo wameweza kujadili kuhusu umuhimu wa kufanya uchunguzi wa
afya wa mapema na kuweka mikakati ambayo itawasaidia waafrika kupambana na
magonjwa yasiyoambukiza.
Kwa upande wake Afisa Uuguzi Mbobezi kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Hania Bwahama alisema wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo watalaamu wa afya na viongozi wa Serikali waliotembelea banda la Taasisi hiyo wamepata fursa ya kujifunza na kuona huduma zinazotolewa na JKCI.
“Katika banda letu tumeweza kuonesha tekinolojia tunazotumia kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo, lakini pia kuonesha vifaa tiba vya kisasa vinavyotumika kufanya uchunguzi na kutibu”, alisema Hania.
Aidha Hania alisema kupitia mkutano huo JKCI imeimarisha ushirikiano na taasisi nyingine za afya na wadau wa maendeleo pamoja na kubadilishana uzoefu na washiriki kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika.
“Mkutano huu umesaidia kuongeza uelewa kuhusu huduma zinazotolewa na JKCI kwa wagonjwa wa moyo wanaotoka katika mataifa mbalimbali ya Afrika kuja kutibiwa JKCI”, alisema Hania.
.jpeg)

.jpeg)
Comments
Post a Comment