Wanafunzi Kibaha wapimwa moyo
Afisa Takwimu wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuelezea Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Kibaha Nyanjige Shimote kuhusu huduma za upimaji wa magonjwa ya moyo kwa watoto alipotembelea Shule ya Sekondari ya Bundikani iliyopo Manispaa ya Kibaha wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika Wilaya ya Kibaha. Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Stella Mongela akimpima mapigo ya moyo kupitia kwenye mkono Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Bundikani iliyopo Manispaa ya Kibaha wakati wa kambi maalumu ya siku mbili ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo ijulikanayo kama Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tiba mkoba katika kuadhimisha miaka kumi ya JKCI inayofanyika katika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani. Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prisca Kiyuka akimpat...